Home LOCAL KATIBU MUHTASI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UFUJAJI, UBADHIRIFU.

KATIBU MUHTASI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UFUJAJI, UBADHIRIFU.

 

SERENGETI.

Katibu Muhtasi katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Vivian Valerian Malasha amefikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Serengeti akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi Namba 84 ya Mwaka 2022.

Wakili  wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), William Lyamboko alisema mbele ya Hakimu Jacob Ndira kwamba kupitia Kesi hiyo, Malasha anashitakiwa kwa makosa ya Ufujaji na ubadhirifu wa Sh milioni 2.160 kinyume na kifungu cha 28 (1) PCCA, kikisomwa pamoja na vifungu vya 57(1) na 60 (2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupanga CAP 200.R.E 2019. 

Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana na kesi imepangwa kwa ajili ya kutajwa tena Julai 06 Mwaka huu.

Previous article“SULUHISHA NA BRELA” YAZIDI KUWAIBUA WAMILIKI WA KAMPUNI
Next articleTIGO YAJA NA SULUHISHO ULIPAJI WA MAEGESHO MLIMANI CITY
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here