Na:WAF – Dar es Salaam
Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) kimetoa wito kwa waandishi wa habari nchini kutoa elimu kwa jamii jinsi ya matumizi sahihi ya dawa ili zisilete madhara na usugu kwa wananchi.
Wito huo umetolewa na Rais wa PST Mfamasia Fadhili Hezekia alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Semina hii kwa waandishi wa habari tunalenga waweze kutumia taaluma hii ya famasi katika utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusiana na Afya hasa tabia ya matumizi holela na yasiyo sahihi ya dawa ambayo zinaleta changamoto katika maswala ya kiuchumi nchini.” amesema Mfamasia Hezekia
Pia, Hezekia ameainisha majukumu ya chama cha wafamasia ikiwa ni pamoja na kutumia weledi, fusra kwa kushiriki kuboresha huduma za upatikanaji wa bidhaa za dAfya Tanzania kwa kushirikiana na wadau kutoka nchini mbalimbali.
Katika kudhihirisha hilo amesema wameandaa maonesho ya kwanza yanayoitwa Farmatech East Africa, katika maonesho hayo bidhaa za Afya za teknolojia za kisasa zitaoneshwa na washiriki zaidi ya 60 watashiriki katika maonesho hayo kutoka Tanzania ma nchi nyingine.
Mfamasia Hezekia amewakaribisha wataalamu,wanafunzi na wananchi katika maonesho hayo yatakayofanyika kuanzia Augusti 30-01 Septemba 2022 jijini Dar es kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.