Home LOCAL CHAMA CHA WAFAMASIA CHAWAKUTANISHA WAANDISHI WA HABARI

CHAMA CHA WAFAMASIA CHAWAKUTANISHA WAANDISHI WA HABARI

Na:WAF – Dar es Salaam

Chama cha Wafamasia Tanzania (PST) kimetoa wito kwa waandishi wa habari nchini kutoa elimu kwa jamii jinsi ya matumizi sahihi ya dawa ili zisilete madhara na usugu kwa wananchi.

Wito huo umetolewa na Rais wa PST Mfamasia Fadhili Hezekia alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Semina hii kwa waandishi wa habari tunalenga waweze kutumia taaluma hii ya famasi katika utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusiana na Afya hasa tabia ya matumizi holela na yasiyo sahihi ya dawa ambayo zinaleta changamoto katika maswala ya kiuchumi nchini.” amesema Mfamasia Hezekia

Pia, Hezekia ameainisha majukumu ya chama cha wafamasia ikiwa ni pamoja na kutumia weledi, fusra kwa kushiriki kuboresha huduma za upatikanaji wa bidhaa za dAfya Tanzania kwa kushirikiana na wadau kutoka nchini mbalimbali.

Katika kudhihirisha hilo amesema wameandaa maonesho ya kwanza yanayoitwa Farmatech East Africa, katika maonesho hayo bidhaa za Afya za teknolojia za kisasa zitaoneshwa na washiriki zaidi ya 60 watashiriki katika maonesho hayo kutoka Tanzania ma nchi nyingine.

Mfamasia Hezekia amewakaribisha wataalamu,wanafunzi na wananchi katika maonesho hayo yatakayofanyika kuanzia Augusti 30-01 Septemba 2022 jijini Dar es kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Previous articleZOEZI LA SENSA GEITA LAFIKIA ASILIMIA 50
Next articleSPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI, SPIKA WA BUNGE LA ZAMBIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here