Home LOCAL BUPE MWAKANG’ATA ACHUKIZWA NA WIZI KATIKA MRADI WA MAJI NKASI, AITAKA WIZARA...

BUPE MWAKANG’ATA ACHUKIZWA NA WIZI KATIKA MRADI WA MAJI NKASI, AITAKA WIZARA KUCHUKUA HATUA KALI

DODOMA.

Serikali imetakiwa kuchukua hatua kwa wezi wanaopelekea miradi ya maji hususani mradi wa Kabwe uliopo katika jimbo la Nkasi kutokukamilika kwa wakati licha ya serikali kutumia gharama kubwa ya fedha kuanzisha miradi na kuiendesha.

Hayo yamesemwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang’ata katika swali lake la nyongeza kwa wizara ya Maji, leo bungeni, jijini Dodoma.

Licha ya serikali kutoa kiasi kikubwa cha fedha, Mbunge Bupe Mwakang’ata amebainisha uwepo wa watu wasiokuwa na nia njema ambao walichukua vifaa muhimu vya kuendeshea mradi huo na hivyo mradi kufanya kazi kwa muda wa miezi mitatu.

“Na mradi huu umefanya kazi kwa miezi mitatu tu, na majizi wakaihujumu miundombinu ya mradi huu kuiba. Sasa serikali inampango gani wa kuwachukulia hatua za kinidhamu”

Mwakang’ata ameipongeza serikali kwa kuingiza jumla ya shilingi bilioni 1.3 ili kukamilisha mradi mkubwa wa maji wa Kabwe uliopo katika jimbo la Nkasi ili kusaidia wananchi wa jimbo  hilo kuondokana na changamoto ya maji.

“Naishukuru serikali imeweza kuingiza kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kwenye mradi huu ili uweze kufanya kazi”

Akijibu swali la mbunge Mwakang’ata, Naibu waziri wa Maji, Eng. Marryprisca Mahundi amesema mradi wa maji Kabwe licha ya kuwa umekamilika lakini umekumbwa na changamoto ya ukosefu wa nishati ya kudumu nyakati zote ya kuendeshea mradi huo hususani wakati wa usiku.

Naibu Waziri Eng. Marryprisca Mahundi amesema serikali imeamua kubadili mfumo wa umeme jua kwenda mfumo wa umeme kutoka kwenye Grid kupitia REA kazi inayotarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Juni, 2021.

“Suala hili hatutazingatia zaidi katika vifaa vya sola tutazingatia kuleta umeme kupitia Grid ya Umeme wa REA ili tuwe na umeme wa uhakika”

Naibu waziri Eng. Marryprisca Mahundi amewatahadharisha watu wasio na nia njema katika miradi ya maji kuacha mara moja nia hiyo kwa kuwa serikali itawachukulia hatua kali za kinidhamu.

“Hawa wezi nenda karipoti polisi, lakini tumemsikia waziri wetu wa maji akisema kama unataka kuchezea mradi wa maji nenda kachezee kitambi chako, hivyo tutawachukulia hatua wezi wote”

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.TANO MEI 26-2021..
Next articleRAIS MWINYI AELEKEA MSUMBIJI KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here