Home INTERNATIONAL JAJI SHINDANO LA BSSA ATANGAZA MAJAJI AMTAJA S2KIZZ

JAJI SHINDANO LA BSSA ATANGAZA MAJAJI AMTAJA S2KIZZ

JAJI Mkuu wa Shindano la kusaka Vipaji Bongo Star Search African ‘BSSA’ Ritha Poulsen ametangaza majaji watakao jaji katika mashindano Projuza S2kizzy Zombi akiwa miongoni mwao.

Akitaja majaji hao wa Bongo Star Search African jijini Dar es Salaam, Madam Ritha amesema kuwa mara zote wamekuwa na wasanii kwa mwaka huu mambo yamebadilika watakuwa na Projuza S2kizzy Zombi.

‘Mashindano ya haya yataongozwa na Kikosi kazi cha majaji watakao jaji msimu wa kumi na tano Jaji Mkuu Ritha Paulsen ‘Madam Ritha’, Johakim Kimario ‘Master J’ Jaji Produza S2KZ Zombi, Salama Jabiri majaji kutoka Nchini Tanzania lakini kutakuwa na majaji wawili watakao jaji kutoka nchini Kenya Sanaipei Tande na Lilian Mbabazi kutokea Uganda”

“Napenda kukukaribisha katika familia ya Bongo Star Search African naamini utakuwa na Mchango mkubwa katika kutafuta vipaji vipya.

“Watangazaji watakao sherehesha msimu wa kumi na tano wa Kipindi cha BSS ni Idris Sultan pamoja na Meena Ally ‘Meena Ally’ wataongoza jahazi la msimu wa kumi na tano hadi watakaofika tamati.“Washiriki wetu, nataka kusema kuwa huu ni wakati wenu.Hii ni nafasi ya kipekee ambayo inaweza kubadilisha maisha yenu.”amesema Madam Ritha

Ushiriki wenu sio tu katika mashindano, bali ni safari ya kujifunza, kukua, na kufikia malengo yenu makubwa.

“Hivyo basi, jiandaeni, aminini katika vipaji vyenu, na wekeni juhudi kubwa katika kila hatua.”amesema Madam Ritha

Kwa upande wake Muandaaji wa kazi za wasanii wa Bongo fleva S2kzzy Zombi amesema kuwa yupo tayari kufanya kazi na BSS na ilikuwa ni ndoto yake ya siku nyingi anaamini watapata vipaji bora zaidi.

“Kwa miaka yangu yote niliyoifanya kazi na wasanii wa kubwa wa ndani na nje ya Tanzania ni imani yangu tutafanya ya kushangaza Afrika.”amesema Zombi

Previous articleDMDP-II KUTUMIA BIL. 290 USIMAMIZI WA TAKA NGUMU
Next articleMTIFUANO MKALI, USAHILI BONGO STAR SEARCH AFRIKA KUANZIA ARUSHA 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here