Home BUSINESS WAZIRI BASHE AKITAKA CHUO KIKUU SUA KUENDESHA MIJADALA YA KILIMO

WAZIRI BASHE AKITAKA CHUO KIKUU SUA KUENDESHA MIJADALA YA KILIMO

NA FARIDA MANGUBE

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema ipo haja ya kuwa na mijadala mahususi ya kitaifa kujadili masuala mtambuka juu ya muundo wa sekta ya kilimo ili kuona namna bora ya kuwezesha kundi la vijana kujihusisha kikamilifu katika shughuli za kilimo.

Aidha Mhe. Bashe amesema taifa linakitegemea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kuendesha mijadala ya aina hiyo kwani ndilo chimbuko la wataalamu wa kilimo na vijana zaidi ya mia mbili wa BBT wanaopelekea kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo kupitia mpango huo.

“Kwa sasa tunawatazama vijana hawa kwa jicho la kipekee kutokana na matokeo ambayo tayari tumekishwa kuanza kuyaona kwao na tuna mpango wa kuwafanya vijana hawa kuwa wao ndio watakao kuwa wanagawa mbegu na pembejeo nyingine kwa wakulima kutokana na kuonesha uaminifu mkubwa kwa serikali “amesema Mhe. Bashe.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Prof. Raphael Chibunda ametumia fursa ya hafla hiyo kuiomba serikali ibadilishe sheria na kanuni za mazingira zinazohusu Bioteknolojia mbegu za GMO ili isiwabane watafiti na kuruhusu watafiti hao kufanya utafiti kwa uhuru ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya kilimo.

“Kanuni zilizopo kwa sasa kupitia sheria ya mazingira zinasema kwamba endapo litatokea tatizo lolote litakalosababishwa na mbegu ya aina hiyo mtafiti atawajibika moja kwa moja juu ya tatizo hilo hali ambayo inawakatisha tamaa watafiti” Prof. Chibunda amesema.

Mhandisi Tito Edimund ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vijana Kilimo Biashara wilaya ya Mvomero amemuomba Mhe. Waziri Bashe kuwa serikali iwawezesha vijana ambao hawamo katika mfumo wa BBT kifedha ili wafanye kilimo chenye tija kuliko ilivyo sasa.

Previous articleWANAHARAKATI WANAOMCHAFUA RAIS SAMIA WAUMBUKA  
Next articleDKT. BITEKO NA WAZIRI WA NYUMBA MISRI KUSIMAMIA UKAMILISHAJI MRADI WA JNHPP
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here