Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya ACB wakijiandikisha tayari kwa kuchangia damu leo kwenye kituo cha redio cha Clouds Mikocheni jijini Dar es salaam. |
Mmoja wa wadau kutoka jijini Dar es salaam akichangia damu katika kampeni hiyo iliyofanyika leo kwenye kituo cha redio cha Clouds Mikocheni jijini Dar es salaam. |
Mtangazaji wa kituo cha Redio cha Clouds Masoud Kipanya akichangia damu katika kampeni hiyo iliyofanyika leo. |
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa akiba Commercial Benki Dora Saria akimsikiliza Masoud Kipanya wakati alipokuwa akizungumza jambo katika kampeni hiyo |
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya ACB wakijaza fomu zao tayari kwa ajili ya kuchangia damu. |
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya ACB wakisubiri kupitia hatua mbalimbali kabla ya kuchangia damu kwenye kampeni hiyo leo. |
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya ACB wakijitolea damu kwenye kampeni iliyofanyika leo katika kituo cha redio cha Clouds jijini Dar es salaam. |
DAR ES SALAAM.
Kama sehemu ya jamii pamoja na kutambua umuhimu wa kuokoa maisha Benki ya Akiba Commercial Benki (ACB) kama taasisi imeshiriki katika zoezi hilo muhimu siku ya leo kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya kuchangia damu ambalo kilele cha maazimisho ni tarehe 14/06/2021.
Jumla ya wafanyakazi takribani kutoka Benki ya ACB wamejitolea kushiriki katika zoezi hilo, kama kutokana na umuhimu wake pamoja na kuguswa mioyoni mwao kama wanajamii na sehemu ya jamii pia kuunga mkono juhudi za Benki katika kushiriki kwenye matukio ya kijamii.
Benki ya Akiba imekuwa mshiriki mahiri katika maswala ya kijamii kwa kutoa misaada katika sekta za Elimu, Mazingira na Afya kama ambavyo imeshiriki katika zoezi hili leo.
Benki hiyo inatoa rai kwa taasisi nyingine na Watanzania wote kwa ujumla kushiriki katika zoezi hili kwa ajili ya kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu wenye uhitaji wa damu ili kuokoa maisha yao ambao wanahitaji msaada huo kutokana na afya zao kutetereka kwa sababu za magonjwa mbalimbali zikiwemo ajali.