Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Seka Kasera, akiwasikiliza wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za BRELA Makao Makuu, zilizopo Jengo la Ushirika Mnazi mmoja, jijini Dar es Salaam. Wateja hawa kila mmoja kwa wakati wake, walipatiwa huduma na Bw. Kasera kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa, ikiwa ni hatua mojawapo ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo tarehe 16 Juni, 2021.