NA: HERI SHAABAN (ILALA)
MWENYEKITI wa Mtaa wa AMANI Kipunguni Wilayani Ilala DANIEL MALAGASHIMBA aamejenga Ofisi ya Serikali ya Mitaa kwa fedha zake.
MALAGASHIMBA alisema ujenzi huo wa Mitaa AMANI Kata ya Kipunguni Wilaya ya Ilala umekamilika kwa asilimia 90 .
MALAGISHIMBA alisema ujenzi wa Ofisi hiyo amejenga kwa nguvu zake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo .
“Tumekakilisha Jengo la ofisi ya Wananchi kwa ajili ya kusaidia Serikali yetu iweze kufikia malengo yake ,jengo hili litafunguliwa hivi karibuni huduma zote za Wananchi zitatolewa hapo huduma ni bure miaka mitatu yote ya uongozi wangu ” alisema Malagashimba.
Alisema Serikali inatakiwa kusaidiwa ili kufikia malengo yake katika kuunga mkono juhudi za Rais wetu Samia Hassan Suluhu kujenga Tanzania ya Uchumi wa Viwanda .
Alisema tukishirikiana tunaweza kwa umoja wetu kujenga Tanzania ya Uchumi wa Viwanda ikiwemo kuokoa fedha za SERIKALI zisipotee bure .
“Wananchi wangu wamekuwa wakipata huduma bure miaka yote ikiwemo na photocopy bure nimesaidia Serikali isilipe kodi ya pango nimetafuta kiwanja kwa nguvu zangu Ofisi ya Serikali za Mitaa bila kuchangisha fedha za wananchi” alisema .
mwisho