Home LOCAL MARAGASHIMBA AJENGA OFISI YA SERIKALI YA MTAA

MARAGASHIMBA AJENGA OFISI YA SERIKALI YA MTAA

 

NA: HERI SHAABAN (ILALA)

MWENYEKITI wa Mtaa wa AMANI Kipunguni Wilayani Ilala DANIEL MALAGASHIMBA aamejenga Ofisi ya Serikali ya Mitaa kwa fedha zake.

MALAGASHIMBA alisema ujenzi huo wa  Mitaa AMANI Kata ya Kipunguni Wilaya ya Ilala  umekamilika kwa asilimia 90 .

MALAGISHIMBA   alisema ujenzi wa Ofisi hiyo amejenga kwa nguvu zake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo .

“Tumekakilisha Jengo la ofisi ya Wananchi kwa ajili ya kusaidia Serikali     yetu iweze kufikia malengo yake ,jengo hili litafunguliwa hivi karibuni huduma zote za Wananchi zitatolewa hapo   huduma ni bure  miaka mitatu yote ya  uongozi wangu ” alisema Malagashimba.

Alisema Serikali inatakiwa kusaidiwa ili kufikia malengo yake  katika kuunga mkono juhudi za Rais wetu Samia Hassan Suluhu kujenga Tanzania ya Uchumi wa Viwanda .

Alisema tukishirikiana tunaweza kwa umoja wetu kujenga Tanzania ya Uchumi wa Viwanda ikiwemo kuokoa fedha za SERIKALI zisipotee bure  .

“Wananchi wangu wamekuwa wakipata huduma bure miaka yote ikiwemo na photocopy bure  nimesaidia Serikali isilipe kodi ya pango nimetafuta kiwanja kwa nguvu zangu Ofisi ya Serikali za Mitaa bila kuchangisha fedha za wananchi” alisema .

mwisho

Previous articleWAZIRI MULAMULA AITAKA STAMICO KUUTANGAZA MKAA MBADALA WA MAKAA YA MAWE.
Next articleMAGAZETI YA LEO J.TATU JULAI 5-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here