Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi shada la mauwa Nd,Pamela Chepkoech kutoka Nchini Kenya akiwa mshindi wa kwanza Wanawake katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Zanzibar International Marathon) ya kilomita 21 alietumia Saa 1:19:50 yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 18/07/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimvalisha nishani Nd,Panuel Mkumbo kutoka Nchini Kenya akiwa mshindi wa kwanza Wanaume katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Zanzibar International Marathon) ya kilomita 21 aliyetumia Saa 1:04:48 yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 18/07/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga bastola juu kuashiria Uzinduzi wa mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Zanzibar International Marathon) ya kilomita 21 zilizoanzia leo katika viwanja vya Ngome Kongwe Mjimkongwe na kumalizia katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 18/07/2021.
Wanariadha katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Zanzibar International Marathon) ya kilomita 21 wakijitayarisha kuanza Mbio hizo leo katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar,ambapo mgeni rasmin alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi(hayupo pichani).[Picha na Ikulu] 18/07/2021.