Home SPORTS RAIS DKT. MWINYI AFUNGUA MASHINDANO YA MBIO ZA MARATHON 2021 ZANZIBAR.

RAIS DKT. MWINYI AFUNGUA MASHINDANO YA MBIO ZA MARATHON 2021 ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi shada la mauwa Nd,Pamela Chepkoech kutoka Nchini Kenya akiwa mshindi wa kwanza Wanawake katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Zanzibar International Marathon) ya kilomita 21 alietumia Saa 1:19:50 yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 18/07/2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimvalisha nishani Nd,Panuel Mkumbo kutoka Nchini Kenya akiwa mshindi wa kwanza Wanaume katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Zanzibar International Marathon) ya kilomita 21 aliyetumia Saa 1:04:48 yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 18/07/2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga bastola juu kuashiria  Uzinduzi wa mashindano ya Kimataifa  ya Riadha (Zanzibar International Marathon)  ya kilomita 21 zilizoanzia leo katika  viwanja vya Ngome Kongwe Mjimkongwe   na kumalizia katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 18/07/2021.

Wanariadha katika mashindano ya Kimataifa  ya Riadha (Zanzibar International Marathon)  ya kilomita 21 wakijitayarisha kuanza Mbio hizo  leo katika   Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar,ambapo mgeni rasmin alikuwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi(hayupo pichani).[Picha na Ikulu] 18/07/2021.
Previous articleYANGA YABANWA MBAVU NA DODOMA JIJI FC, WATOKA SARE 0-0
Next articleMBUNGE BONAH KUSHIRIKIANA NA MADIWANI KUIBUA VIPAJI SEGEREA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here