Home SPORTS YANGA YABANWA MBAVU NA DODOMA JIJI FC, WATOKA SARE 0-0

YANGA YABANWA MBAVU NA DODOMA JIJI FC, WATOKA SARE 0-0

 
DAR ES SALAAM.

KLABU ya Yanga imeshindwa kutoka na ushindi dhidi ya timu ya Dodoma Jiji katika mchezo wa kufunga ligi kuu bara mchezo ambao ulipigwa katika dimba la Jamhuri Jijini Dodoma.

Yanga ambayo ilikuwa imeshajihakikishia nafasi ya pili kwenye ligi iliweza kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji wao na  wengine wakipumzishwa kutokana na mchezo mkali unaofuata wa fainali dhidi ya mahasimu wao Simba Sc utakaopigwa Julai 25 mwaka huo mkoani Kigoma.

Klabu ya Yanga sasa itakuwa inashika nafasi ya pili ikikusanya pointi 74 katika michezo 34 ya ligi kuu bara, huku Dodoma Jiji  ikijikusanyia pointi 44 ikishika nafasi ya nane kwenye ligi.

 

Previous articleSIMBA YAKABIDHIWA RASMI KOMBE LA UBINGWA WA LIGI KUU, YAIPIGA NAMUNGO 4-0 KWA MKAPA
Next articleRAIS DKT. MWINYI AFUNGUA MASHINDANO YA MBIO ZA MARATHON 2021 ZANZIBAR.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here