Na: Saimon Mghendi,KAHAMA.
Mkurugenzi wa Manispaa ya kahama Anderson Msumba, Amewataka wafanyabiashara wote wanaofanya biashara nje ya soko la majengo kuamia ndani ya soko hilo amablo limekarabatiwa na halmashauri ya manispaa ya Kahama na kutumia Zaidi ya tsh. Mil 200.
Msumba ameyasema hayo leo wakati akikabidhi hati ya soko kwa uongozi mpya wa soko la majengo lililoopo kata ya majengo, katika Manispaa ya Kahama, ambapo aliwataka viongozi wa mtaa na kata kuakikisha wanatumia njia rafiki kuwaondoa wafanyabiashara wote waliopo nje ili waweze kufanya biashara ndani ya soko.
Hata hivyo Msumba amesema kuwa serekali imeweka umeme katika soko hilo ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara mpaka usiku na kuwataka wajasiriamali ambao hawana mitaji kuja kuoomba mkopo.
Kwa upande wake Katibu wa soko Agnes Jonathan ambaye ni mojawapo wa viongozi wapya wa soko hilo, Ameishukuru Serekali ya Manispaa ya Kahama kwa kukarabati soko hilo na kusema wao kama viongozi watashirikiana bega kwa bega na serekali.
Naye Mwenyekiti wa wauza Mboga mboga, Angel Charles kwa niaba ya wajasiriamali wengine ameishukuru serekali kupitia mkurugenzi kwa kutatua changamoto zao.