Home LOCAL TANZANIA YAPOKEA ZAIDI YA DOZI MILIONI 1 YA CHANJO YA COVID-19 KUTOKA...

TANZANIA YAPOKEA ZAIDI YA DOZI MILIONI 1 YA CHANJO YA COVID-19 KUTOKA MAREKANI

DAR ES SALAAM.

Serikali ya Tanzania, imepokea zaidi ya dozi milioni moja za chanjo ya Covid-19 kutoka nchini Marekani, kupitia Mpango wa Usambazaji Chanjo wa Covax kwa uratibu wa Umoja wa Afrika (AU).

Chanjo hiyo imepokelewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Liberata Mulamula katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright kupitia akaunti ya ubalozi wa Marekani Twitter, amesema kuwasili kwa chanjo hiyo ni kielelezo cha uimara wa ubia wetu wa miaka 60 na dhamira yetu ya dhati kwa Tanzania.
Previous articleMKURUGENZI MANISPAA YA KAHAMA AAGIZA WAFANYABIASHARA WALIOKO NJE YA SOKO LA MAJENGO KUHAMIA NDANI YA SOKO HILO
Next articleMAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AWEKA JIWE LA MSINGI SOKO LA KISASA JIDA MJINI MASASI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here