Home BUSINESS DAWASA NA TARURA KUENDELEZA USHIRIKIANO ULINZI WA MIUNDOMBINU

DAWASA NA TARURA KUENDELEZA USHIRIKIANO ULINZI WA MIUNDOMBINU

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekutana na kufanya mazungumzo na Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) Mkoa wa Dar es salaam yaliyolenga kuangalia njia bora ya kushirikiana katika ulinzi na utunzaji wa miundombinu katika Jiji la Dar es salaam.

Akiongea katika kikao kazi hicho, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire ameeleza kuwa TARURA ni wadau muhimu sana na kwa pamoja hushirikiana na DAWASA katika utekelezaji wa kazi zao.

“DAWASA tupo tayari kushirikiana kwa karibu sana na TARURA, tunaomba kipindi cha utekelezaji wa miradi ya TARURA hasa ukarabati wa barabara tuweze kupeana taarifa mapema ili kuweza kuondoa miundombinu ya maji na kuzuia uharibifu” ameeleza Mhandisi Bwire.

Kwaupande wake Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es salaam Mhandisi Geofrey Mkinga ameishukuru DAWASA kwa ushirikiano na kusema kwamba wamejipanga kikamilifu kushirikiana na DAWASA katika kutekeleza malengo makuu ya Serikali ya kuwapatia wananchi huduma pamoja na utunzaji wa pamoja wa miundombinu.

 

Previous articleTAKUKURU ARUSHA YAWAFUNDA WANAHABARI MADHARA YA RUSHWA KWENYE UCHAGUZI.
Next articleWAZIRI MAVUNDE AGEUKA MBOGO; ATAKA MRADI WA DHAHABU MAGAMBAZI UZALISHAJI MKUBWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here