Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi ameipongea Wizara ya Uwekezaji na Biashara kwa kuanzisha Mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja kwa wawekezaji na programu ya utengenezaji wa mashine mbalimbali zinazowezesha uanzishaji wa viwanda .
Rais Mwinyi ameyasema hayo Julai 04 2022 alipotembelea Banda la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara nakujionea Mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja kwa wawekezaji na mashine mbalimbali zinazoweza kutumika kuanzisha kiwanda kuanzia milioni sita hadi milioni 600.
Rais Mwinyi amesema hii ni hatua nzuri kwani hata nchi zilizoendelea zilianza kutengeneza mashine kama hizi na sasa zinatengeneza mashine na mitambo mikubwa. Natumaini mwakani mtakuwa na maendeleo makubwa ya mashine hizo.