Home BUSINESS SERIKALI YATOA MSAMAHA WA ADA NYARAKA ZA KAMPUNI NJE YA MUDA

SERIKALI YATOA MSAMAHA WA ADA NYARAKA ZA KAMPUNI NJE YA MUDA

Dar es Salaam-4 Juni, 2024

Serikali ametoa Notisi ya Msamaha wa asilimia hamsini (50%) ya ada ya uwasilishaji wa nyaraka za kampuni nje ya muda iliyotolewa katika Tangazo la Serikali Na. 410 la tarehe 24 Mei, 2024 na itatumika kwa kipindi cha miezi kumi na mbili tangu kuchapishwa kwake.

Kufuatia taarifa ya Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji iliyoyolewa leo Juni 4,2024 na Msajili wa Kampuni na Leseni (BRELA), imeeleza kuwa Waziri ametoa Notisi hiyo kwa kuzingatia kifungu cha 452A cha Sheria ya Kampuni, Sura ya 212 kinachotoa Mamlaka kwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya biashara kutoa msamaha wa ulipaji wa ada ya uwasilishaji wa nyaraka za kampuni nje ya muda.

“Notisi hii imetolewa kwa lengo la kuwezesha uhuishaji wa taarifa za kampuni zilizosajiliwa kabla ya mwaka 2018 kwenye mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandaoni (Online Registration System)”  imeeleza taarifa hiyo.

Kufuatia notisi hiyo, Msajili wa Kampuni anawataarifu wadau na Umma kwa ujumla kuwa msamaha wa asilimia hamsini (50%) unatolewa kwa ada ya ucheleweshaji wa nyaraka (late filing fee) kwa Kampuni zenye sifa zifuatazo;

a) Kampuni zilizosajiliwa kabla ya mwaka 2018 ambazo taarifa zake hazijahuishwa kwenye Mfumo wa Usajili wa Kampuni kwa njia ya Mtandao,

b) Maombi ya kuhuisha taarifa za kampuni yaliyopo kwenye Mfumo wa usajili wa kampuni kwa njia ya Mandao kabla ya tarehe ya kuchapishwa kwa Notisi hii,

c) Maombi ya kuhuisha taarifa za kampuni kwenye Mfumo wa Usajili wa Kampuni kwa njia ya Mtandao yatakayopokelewa kwenye Mtandao ndani ya muda wa Notisi hii.

Aidha, ifahamike kwamba maombi yaliyokwisha wasilishwa kwenye Mfumo na kupitishwa na Msajili au Msajili kuingia makubaliano yoyote na Kampuni husika ya jinsi ya kufanya malipo husika kabla ya terehe ya Notisi hayatahusika na msamaha huu.

Msajili anazielekeza Kampuni zote zinazohusika na Msamaha huu kuwasilisha taarifa zao kwa Msajili kupitia mfumo wa ORS ndani ya muda ulioelekezwa ili kunufaika na msamaha huo.

Previous articleOCEAN ROAD YAPIGA KAMBI KITUNDA UCHUNGUZI WA SARATANI
Next articleWAJASIRIAMALI WADOGO WAPATA ELIMU YA FEDHA SUMBAWANGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here