Timu ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiongozwa na Mtaalam wa Mawasiliano Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Bi. Zuhura Mdungi wakikagua ujenzi wa nyumba ya watumishi iliyojengwa na TASAF katika Zahanati ya Mtaa wa Ramadhan Halmashauri ya Mjombe mkoani Mjombe wakati wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko huko mkoani humo.
Ukaguzi wa nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Mtaa wa Ramadhan mjini Njombe ukiendelea.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa nyumba ya watumishi wa zahanati katika mtaa wa Ramadhani Halmashauri ya wilaya ya Njombe Bashir Nyapini Sanga akizungumza kuhusu mradi huo.
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Ramadhani Bi Rehema Omari akifafanua jambo mbele ya Wahariri waliotembelea mradi huo.Â
………………………Â
NA JOHN BUKUKU NJOMBE.Â
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa nyumba ya watumishi na zahanati katika mtaa wa Ramadhani Halmashauri ya wilaya ya Njombe Bashir Nyapini Sanga ameushukuru Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa kukamilisha ujenzi wa mradi huo has a nyumba ya watumishi ambayo itaanza kutumika hivi karibuni.Â
Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini waliopo kwenye ziara ya kutembelea miradi ya TASAF mkoni mkoani Mjombe amesema kukamilika kwa nyumba hiyo ya watumishi kutasaidia kupunguza changamoto wanazozipata wagonjwa hasa wanapoumwa wakati wa usiku wakiwemo wakimama wajawazito pindi wanapotaka kujifungua.
“Kukamilika kwa nyumba ya mganga itawasaidia mama zetu wanapokuja hapa kituoni kupata huduma stahiki na kwa wakati lakini pia itaondoa kero ambayo anaipata mganga kukaa mbali na kituo kunakopelekea kuamshwa usiku kutoka alipo mpaka hapa kituoni ambapo kunaumbali”amesema.
Aidha amesema kuwa TASAF iliingiza fedha kiasi cha shilingi milioni 66,591,375.89 kwa ajili ya kusapoti mradi huo lakini haikutosha hali iliyopelekea kuongezewa tena fedha kiasi cha shilingi milion 15.
“Mradi huu mpaka ninavyozungumza umegharimu kiasi cha shilingi milioni 81,591,375 ambapo mpaka sasa imetumika shilingi milioni 78,716500 lakini kwenye mradi huu nguvu kazi ya umma ambayo kukiithaminisha na fedha gharama yake inakua milion 8,76,000 “amesema
Akizungumzia changamoto amesema mpaka kufika hapo ulipofika hakuna changamoto kubwa waliyokutana nayo ambayo imeshindwa kutatuliwa na kamati kwa kushirikiana na serikali ya mtaa.
“Changamoto kubwa tuliyokutana nayo ni kusita sita kwa wazabuni kufanya kazi kwa madai ya kucheleweshewa fedha na kutokana na utaratibu wa malipo ya serikali “amesema.
Kwa upande wa mganga mfawidhi wa zahanati ya Ramadhani Bi Rehema Omari amesema ujenzi wa nyumba za wahudumu wa afya utawasaidia kutoa huduma za dharura hasa kwa wakinamama wajawazito ambao wanafika kituoni hapo kwa ajili ya kupata huduma.
“Asilimia kubwa ya wajawazito uchungu unaanza jioni lakini kutokana na changamoto tuliyonayo hapa watumishi tulikuwa hatuishi karibu na zahanati lakini pia zahanati haina uwezo wa kulazza wagonjwa zaidi ya kupumzishwa kwa saa12 lakini tutakapo kua tunakaa hapa tutapata nafasi nzuri ya kuwahudumia wananchi”amesema.
Sambamba na hayo Dkt. Rehema ameiomba TASAF kusaidia kukamilisha ujenzi jengo la mama na mtoto ili kuzuia kero inayotokana na kukosa chumba cha kutosha cha kuwasaidia wajawazito ambapo sasa hivi chumba ni kidogo kinachoweza kumsaidia mjamzito mmoja tu ambapo kwa muda wa mwezi mmoja wanawazalisha akinamama 10 ambao wanaenda kujifungua katika zahanati hiyo.
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Ramadhani Bi Rehema Omari akimpima presha mhariri kutoka ETV na EFM Bi. Scholastica Mazula katika Zahanati hiyo ambayo pia imejengwa na TASAF.
Wahariri wakipata maelezo wakati walipokagua nyumba ya watumishi ya Zahanati ya Mtaa wa Ramadhan.
Muonekano wa nyumba mpya ya watumishi ya Zahanati ya Mtaa Ramadha mjini Njombe.Â
Hili ndiyo jengo la Zahanati ya Mtaa wa Ramadhan mjini Njombe.Â