Home SPORTS YANGA SC MGUU SAWA CAF

YANGA SC MGUU SAWA CAF

DAR ES SALAAM 

Mabingwa watetezi Ligi Kuu ya NBC KLABU ya Yanga imfanikiwa kuondoka na alama tatu katika mchezo wake dhidi ya Medeama katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
 
Katika mchezo huo ambao Yanga imepata ushindi wa wa mabao 3-0, mchezo ulikuwa na umuhimu mkubwa kwa Yanga ili kufufua matumaini ya kufuzu Robo Fainali.
 
Mabao ya Yanga yamewekwa kimyani na kiungo wao nyota Pacome Zouzou, bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
 
Medeama ilipata bahati ya kupata faida ya mkwaju wa penati mara baada ya mshambuliaji wao Sowah kuchezewa rafu na mlinzi wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto lakini penati haikuzaa matunda kwao kwani Kipa wa Yanga Djidji Diara kufanikiwa kuokoa mkwaju huo wa penati.
 
Mabao mengine ya Yanga yamefungwa kipindi cha pili na Bakari Mwamnyeto pamoja Mudathir Yahya.
 
Yanga Sc sasa itakuwa inashika nafasi ya pili kwenye kundi lao ambalo linaongozwa na Al ahly ya Cairo
Previous articleTMDA YAKAMATA WACHEPUSHAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA VYA SERIKALI
Next articleTASAF YAJENGA NYUMBA YA MADAKTARI ZAHANATI YA RAMADHAN MKOANI NJOMBE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here