Home BUSINESS WATANZANIA WAHAMASISHWA MATUMIZI YA KIDIJITALI KWENYE MALIPO

WATANZANIA WAHAMASISHWA MATUMIZI YA KIDIJITALI KWENYE MALIPO

Na: Esther Mnyika

Lake Energies kwa kushirikiana na M-pesa watachangia kusaidia juhudi za serikali za kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidigitali kwa kurahisisha watanzania wengi kubadilika kwenye malipo ya kidigitali na kuachana kubeba pesa taslimu ambayo inaweka usalama wao.

Hayo amebainishwa leo Disemba 20 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Oparesheni za M-pesa Vodacom, Titi Mbise amesema kuwa hiyo ni sehemu ya mkakati wa M-pesa kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidigitali kuhakikisha usalama,urahisi katika shughuli za biashara.

Amesema katika jitihada endelevu za kuchochea uchumi malipo kidigitali wateja wote wa lake Energies wanaweza kulipia kwa simu ya mkononi kwa M-pesa kutoka Vodacom katika vituo vyote vya mafuta nchi nzima.

“Kupitia ushirikiano huu ni kurahisisha malipo ya wateja asilimia 10 ya malipo yao ya mafuta wanapofanya malipo kupitia M-pesa siku za ijumaa na jumapili kuanzia msimu wa sikukuu hadi Januari mwakani na tunanaelewa watu wengi wanasafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kuwatembelea wapendwa wao wakati huu suluhisho la malipo ni kidigitali ni wakati mwafaka,”amesema Mbise.

Ameongeza kuwa ikiwa inahudumia soko la Tanzania kwa miaka 15 sasa M-pesa inajivunia kuwa na mtandao mpana wa wafanyabiashara wapato 275000 nchini kote na imejikita katika kurahisisha maisha ya kila siku ya wateja wanaendelea na ubunifu.

Naye Mkurugenzi wa Huduma Rejareja wa Lake Energies Nchini, Fredy Mchau amesema dhamira yao daima imekuwa kuhakikisha wateja wanaotembelea vituo vyao wanapata huduma chaguzi mbalimbali za malipo.

“Ushirikiano huu na kampuni inayojitolea kutoa suluhisho za malipo kidigitali ni hatua muhimu kuelekea katika lengo hili na huduma zinapatikana Lake Energies katika vituo 139 nchini kote,”amesema Mchau

Mwisho

Previous articleTASAF YAJENGA NYUMBA YA MADAKTARI ZAHANATI YA RAMADHAN MKOANI NJOMBE
Next articleBALOZI MBAROUK ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA KUWAIT
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here