Home BUSINESS KAMPUNI YA ORYX GAS YAWAWEZESHA MAMA LISHE NISHATI SAFI YA KUPIKIA

KAMPUNI YA ORYX GAS YAWAWEZESHA MAMA LISHE NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Na Mwandishi Wetu,Rufiji

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imesema katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022 mpaka sasa Desemba 2023 wameshagawa bure mitungi ya gesi na majiko yake zaidi ya 15000 katika makundi mbalimbali ya wananchi ambapo katika mpango huo wameshatumia Sh.bilioni moja huu mkakati wao ni kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman ( katikati) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania( UWT) Marry Chatanda( wa pili kulia), Katibu Mkuu wa UWT Jokate Mwegelo(wa tatu kulia) , Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa(wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa Oryx na jiko lake mmoja wa Mama Lishe wa Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani( wa tatu kushoto), lengo ni kuwawezesha Mama Lishe kutumia nishati safi ya kupikia badala ya kuni na mkaa.Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa Oryx Peter Ndomba na kulia ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa Pwani Zainab Vullu.Jumla ya mitungi 900 ya Oryx Gas na majiko yake yametolewa bure kwa Mama Lishe wote wa Wilaya hiyo

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman katika Kata ya Kikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati wa sherehe za kukumbuka mchango wa mwanama Shupavu Bibi Titi Mohamed ambaye enzi za uhai wake ametoa mchango mkubwa katika kupigania ukombozi wa Taifa hili sambamba na kuwapinia wanawake wa Tanzania.

Hivyo katika kukumbukka mchango wa Bibi Titi , Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ameamua kushirikiana na Oryx Gas kuhakikisha wanafanikisha Mama Lishe kupatiwa mitungi hiyo ili kuwarahisishia shughuli zao za kila siku sambamba na kulinda afya na mazingira.

.”Oryx Gas kuanzia mwaka 2022 mpaka leo hii tumeshagawa mitungi ya gesi na majiko yake 15000 na katika kufankisha hilo tumetumia Sh.bilioni moja za Tanzania na mkakati wetu ni kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kugawa mitungi ya gesi kwa makundi mbalimbali.

“Tumefurahi kuleta nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa wilaya ya Rufiji na kugusa kundi hilo muhimu la Mama Lishe ambalo shughuli zao za kila siku zinahitahi kupata nishati ya kupikia. Kupika katika gesi ya oryx ni kulinda mazingira kwa kuacha kukata miti na zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake na watoto ambao wamekuwa wakiathirika kwa kuvuta moshi mbaya unaotokana na kuni.

” Rais wetu Mama Samia amejipanga kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata nishati safi ya kupikia ifkapo 2032. Katika mkutano wa Dubai ,Rais Samia amezindua Mpango wa Nishati safi ya kupikia kwa wanawake wa Afrika.Oryx Gas tutaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhamasisha matumizi ya nishati safi ua kupikia kwa kugawa bure mitungi ya gesi na majiko yake.Ahadi yetu kwa Serikali tutaendelea kuhamasisha kwa kugawa bure mitungi na majiko kwa makundi mbalimbali ya wananchi.”

Akieleza zaidi amesema kutumia nishati safi ya kupikia kunafaida kubwa za kiafya na kimazingira lakini wakati huo huo inatoa nafasi kubwa ya watoto kupata nafasi ya kwenda shule kupata elimu badala ya kutumia muda mwingi kwenda kukusanya kuni.”Nakushukuru Waziri Mchengerwa kwa kufanikisha mpango huu wa nishati safi ya kupikia kwa wnanchi wa Rufiji kwa kuwapatia mitungi ya gesi 900.

Awali Waziri Mchengerwa amesema matumizi ya kuni na mkaa yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira na kusababisha kero mbalimbali, hivyo kutumia nishati safi ya kupikia kutapunguza uharibu wa maazingira lakini pia kulinda afya za wanawake na watoto ambao ndio waathitika wakubwa wa moshi wa kuni wakati wa kupika.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania( wa tatu kushoto) akikimkabidhi mtungi wa gesi ya Oryx na jiko lake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) Marry Chatanda(wa pili kulia) na Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa( wa tatu kulia).Mitungi hiyo imekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa UWT kabla ya kuanza kuigawa kwa Mama Lishe wote wa Wilaya ya Rufiji ambapo jumla ya mitungi 900 ya gesi ya Oryx na majiko yake imekabidhiwa kwa mamalishe.Wengine wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu UWT Jokate Mwegelo( kushoto) , Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wanu Hafidh Ameir( wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Zainab Vullu( kulia)

Amefafanua aumuzi wa kugawa mitungu kwa Mama lishe wote wa wilaya ya Rufiji unalenga kutambua mchango mkubwa wa wanawake wa jimbo hilo katika kujiletea maendeleo na kutunza mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia na kuachana na kutumia kuni.

“Tunatambua mchango mkubwa wa kundi hili la mama zetua na dada zetu ambao wanajihusisha na shughuli za Mama Lishe, hivyo kwa kushirkiana na viongozi wenzangu wakiwemo madiwani tulikubabaliana tutafute mitungi ya gesi ya orxy na kisha kuwapatia mama lishe wote wa wilaya ya Rufiji wako 1300 .Hivyo leo kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx tunagawa bure mitungi 900 yakiwa na majiko yake bure na mitungi iliyobakia tutagwa hivi karibuni.

“Tunataka kuona Mama Lishe wa wilaya ya Rufiji wanakuwa sehemu ya kutunza mazingira kwa kupikia nishati safi lakini wakati huo huo kuwalinda dhidi ya athari zinazotokana na kuvuta moshi wa kuni wakiwa katika shughuli zao za kila siku,”amesema Mchengerwa huku akisisitiza kuwa umefika wakati wa wananchi kuungana na Serikali inayoongozwa na Rais Samia katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuendelea kulinda mazingira yetu.

Wakati huo huo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Pwani, Jenipher Shirima, ametumia nafasi hiyo kuelezea kwa kina kuhusu namna nzuri ya kutumia nishati ya gesi katika kupikia ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea iwapo itatumika vibaya.

“Ni muhimu kwa wanawake na wananchi wote kuzingatia matumizi bora ya majiko ya gesi na kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto na pale yanapotokea kutoa taarifa mapema kwa jeshi hilo hatua zichukuliwe haraka.

Previous articleADAM MIHAYO ATAMBULISHWA RASMI KUANZA MAJUKUMU YAKE  TCB
Next articleWADAU WANAOPINGA UKATILI WA KIJINSIA,KUENDELEA KUELIMISHA JAMII

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here