Home Uncategorized TAASISI YA TOMA KUWALETA WAANDISHI WA HABARI ZA MITANDAO

TAASISI YA TOMA KUWALETA WAANDISHI WA HABARI ZA MITANDAO

Na: Mwandishi wetu

Taasisi ya Tanzania Online Media Alliance (TOMA) imewataka waandishi wa habari za mtandaoni nchini kujiunga kupitia mwavuli wa taasisi hiyo ili kujijenga kitaaluma, na kuwa na sekta moja ya waandishi wa habari za mtandaoni yenye sauti moja ya kutetea maslahi yao.

Akizungumza leo Novemba 22 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mpango mkakati huo Mkurugenzi wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC,) Kenneth Simbaya amesema kuwa katika kuyafikia malengo ni muhimu waandishi wa habari kufanya kazi kwa manufaa ya Umma pamoja na kuzingatia sheria na kanuni hususani katika wakati huu ambao Sayansi na Teknolojia inakua kwa kasi.

Amesema, Uzinduzi wa mpango mkakati huo wa mtandao wa waandishi wa habari za mtandaoni umelenga kuwaunganisha wanahabari hao pamoja na kuwajengea uwezo wa kuandika habari zinazoendana na wakati na kuzingatia ubora wa matumizi kwa Umma wa watanzania.

“Sayansi na Teknolojia inakua kwa kasi, lazima tuzingatie nidhamu katika kufikisha ujumbe kwa jamii pamoja na kuzingatia weledi na sheria za habari…nazipongeza klabu za waandishi wa habari za mikoa yote kwa jitihada mnazochukua katika kuimarisha zaidi tasnia hii ya habari hususani klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha ambako imetoka taasisi hii ya TOMA,”amesema Simbaya.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Freedom House, Daniel Lema amesema kuwa, lengo na kuzindua mpango mkakati huo ni kutoa mwelekeo wa namna ya utekelezaji wa shughuli za taasisi ya TOMA kwa miaka mitano ijayo.

“Mtandao huu kwa waandishi wa habari za mtandaoni umelenga kuwaunganisha wanahabari hao na kuwa na sauti moja na kutetea maslahi yao kote nchini kama sekta moja ya waandishi wa habari za mtandaoni,” amesema Lema.

Aidha ameeleza kuwa TOMA imelenga kuboresha habari zinazotolewa na waandishi wa habari za mtandaoni kwa kuhakikisha zinahusisha sauti za pembezoni ambazo hazisikiki katika uga huo ikijumuisha makundi mbalimbali ikiwemo asasi za kiraia na watu waliopo pembezoni ambako sauti zao hazisikiki na kuhakikisha zinaletwa katika uga wa habari za mtandaoni.

Ametoa mwito kwa waandishi wa habari za mtandaoni kujiunga na chombo hicho ambacho kimeundwa kwa ajili yao na kuwataka wajiunge kwa manufaa ya kujijenga kitaaluma, kutoa na kujibu changamoto zinazowakabili.

Mmoja ya wanachama wa TOMA na Mkurugenzi wa Kijukuu Blog kutoka Kahama, William Bundala amesema, uzinduzi huo wa mpango mkakati wa miaka mitano ijayo ni fursa kwa wanahabari za mtandaoni kwa kuwa inawaleta pamoja na kubadilishana uzoefu.

“Waandishi wa habari habari za mtandaoni tupo wengi, na kupitia TOMA tunaamini wanahabari wengi zaidi watajiunga katika idadi ya wanachama 260 tuliyopo ili kujenga zaidi tasnia hii ya habari za mtandaoni kwa kuzingatia sheria na kanuni za habari,” amesema Bundala.

Mwisho.

Previous articleNISHATI YAONGOZA KAMATI YA BUNGE NCHINI INDIA
Next articleTIKA YAZINDUA MAONESHO YA KAZI ZA SANAA ZA ALBAYRAK KALIGRAFI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here