Home LOCAL TIKA YAZINDUA MAONESHO YA KAZI ZA SANAA ZA ALBAYRAK KALIGRAFI

TIKA YAZINDUA MAONESHO YA KAZI ZA SANAA ZA ALBAYRAK KALIGRAFI

Dar es salaam Maonesho ya michoro ya maandishi “kaligraphy” yamezinduliwa na Naibu Spika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma, ambapo amesema ushiriano kati ya Nchi ya Tanzania na Uturuki katika mambo ya kijamii,hivyo wameona ni muhimu kwa wasanii wachoraji wa maandishi ndani na nje ya Nchi kuja kuona sanaa kazi hii ya sanaa wanayoifanya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Novemba 21- 26 jijini Dar es salaam Naibu Spika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni amesema sanaa ni njia moja ya kutambuana hivyo hutoa fursa ya kuheshimiana, tamaduni tofauti hupelekea kujenga mahusiano ya kibinaadam yanayosaidia kujenga amani na maelewano.

“Pia hili jambo ni zuri kubadilishana tamaduni ni njia moja wapo ya kutambuana, kila moja kati yetu ana utamaduni wake, tunapojifunza tamaduni za wengine inamaana tunaanza kujenga mahusiano ya kibinaadam yanasadia kuishi katika dunia yenye amani na mshikamano” amesema Mgeni

Nae Mkurugenzi wa taasisi ya Shirika la Uturuki TIKA lilosimamia ufadhili wa onesho hilo amesema wataendelea kutumia sanaa kutunza umoja na mshikamano sio tu baina ya Tanzania na Uturuki pamoja na sehemu zingine duniani.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji bodi ya filamu Tanzania Dk Kiagho Kilonzo ameeleza nia ya Uturuki kuongeza mahusiano na Tanzania ya kitaaluma upande wa filamu kwa kutoa mafunzo ya filamu na ufundi kwa Watanzania ikizingatiwa  Uturuki ni nchi inayofanya vizuri kwenye tasnia hiyo 

 

 

Previous articleTAASISI YA TOMA KUWALETA WAANDISHI WA HABARI ZA MITANDAO
Next articleGGML, CCBRT WAKABIDHI VITIMWENDO 55 KWA WENYE ULEMAVU GEITA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here