Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Mwanga Hakika Microfinance Limited Projest Massawe (katikati) akiwa na Katibu wa Benki hiyo Nancy Kissanga (Kushoto) na Elifuraha Charles (kulia) Katika mkutano wao na waandishi wa habari kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa wanahisa wa Benki hiyo utakaofanyika Septemba 18, Mwanga Kilimanjaro. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki hiyo Projest Massawe Akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) Katika mkutano wao uliofanyika kwenye Ofisi za Benki hiyo Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Mwanga Hakika Microfinance Limited Projest Massawe (kulia) akisisiza jambo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye mkutano huo. (Kushoto) ni Katibu wa Benki hiyo Nancy Kissanga. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
Benki ya Mwanga Hakika Microfinance Limited imesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake imeweza kuwafikia wananchi kwa kuongeza idadi ya mawakala zaidi na kufungua matawi mapya nchini.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki hiyo Projest Massawe katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ofisi za Benki hiyo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia Mkutano Mkuu wa wanahisa wa Benki hiyo unaotarajiwa kufanyika Septemba 18, mwaka huu.
Projest ameeleza kuwa mkakati wa Benki hiyo ni kuwafikia wateja wengi zaidi kwa kutumia njia mbalimbali zikiwemo mawakala ambao mpaka Sasa wapo zaidi ya 50 nakwamba kwa mwaka huu wataongeza mawakala wengi zaidi.
Akizungumzia mkutano mkuu wa wanahisa Massawe amesema kuwa mkutano huo utafanyika Katika Wilaya ya Mwanga Mkoani kilimanjaro na maandalizi yote yamekamilika.
“Benki yetu itakuwa na Mkutano wa kwanza na wanahisa wake ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Makampuni ambayo inazitaka Kampuni au Taasisi kuwa na mikutano ya Mwaka ya wanahisa ujadili Mambo mbalimbali ya mwenendo wa Taasisi” amesema Projest.
Aidha ameongeza kuwa mkutano huo utahudhuriwa na watu wachache kwenye ukumbi na wengine watajiunga kwa njia za mtandao ‘Video Conference’, ikiwa ni matokeo ya hatua za kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu wa Covid-19.
Kufanyika kwa mkutano huo kunatoa fursa kwa wanahisa wa Benki hiyo kuweza kujadili mwenendo wa Benki yao na kuona namna gani watakavyoweza kupata gawio la faida kulingana na watakavyokubaliana.