Home SPORTS DJUMA SHABAN, AUCHO NA FISTON KUIKOSA RIVERS UTD.

DJUMA SHABAN, AUCHO NA FISTON KUIKOSA RIVERS UTD.

Stella Kessy,Dar es Salaam.

UONGOZI  wa Yanga umethibitisha kuwakosa wachezaji  wake watatu kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United utakaopigwa  Septemba12 mwaka huu.

Akizungumza leo katika klabu yao,Ofisa habari wa klabu ya  Yanga, Haji Manara amesema  kwamba Yanga itawakosa wachezaji watatu ambao ni kiungo Khalid Aucho, beki Djuma Shaban na mshambuliaji Fiston Mayele.

Manara amesema kukosekana kwa wachezaji hao hakuna makosa yoyote ya klabu yao ambapo matatizo hayo yamesababishwa na makosa ya klabu walizotokea kushindwa kuachia hati za uhamisho (ITC).

Aliongeza kuwa “Yanga ilifanya kila kitu kwa wakati katika kuomba hati za uhamisho mchezaji kama Khalid Aucho alikuwa na mgogoro na klabu yake hawakumlipa mishahara yake na FIFA wakamvunjia mkataba na kuwa mchezaji huru,”

“Djuma Shaban naye tuliomba vitu vyote kwa wakati lakini klabu yake wakatoa ITC siku moja baada ya dirisha kufungwa hapo Yanga inakosa gani”
Alihoji Manara.


Aidha Manara ameongeza kwamba kutokana na changamoto hizo tayari uongozi wa klabu yao wamewasiliana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF ) kuwaomba FIFA kuingilia kati hatua hiyo.

“Tunaamini wenzetu wa Fifa watatupa majibu mazuri lakini hata hivyo Yanga imejiandaa vizuri na kikosi ni kipana wapo wachezaji hata wakikosekana hao wapo ambao wataziba nafasi zao.” Amesema Manara.

Anasema kuwa mipango ipo sawa na wanaamini kwamba kwenye mashindano ya kimataifa watafanya vizuri.

Alifafanua kuwa Septemba 12, Uwanja wa Mkapa Yanga itasaka ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Rivers United ya Nigeria.
Manara amesema kuwa:”Tuna amini kwamba sisi tuna mipango mizuri na tunahitaji kufika hatua ya makundi haitakuwa kazi rahisi ila inawezekana kwa msaada wa Mungu.”Kikubwa

“mashabiki tuzidi kuwa na ushirikiano na wachezaji wao kazi yao ni kusaka ushindi na kutupa furaha ambayo tunahitaji kupata ushindi,” amesema.

Previous articleKIKOSI CHA SIMBA SASA KAMILI, WACHEZAJI WOTE KUREJEA KAMBINI LEO.
Next articleBENKI YA MWANGA HAKIKA LTD KUFANYA MKUTANO WAKE WA KWANZA WA WANAHISA SEPTEMBA18,2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here