Home SPORTS SIMBA NA COASTAL HAKUNA MBABE

SIMBA NA COASTAL HAKUNA MBABE

Mwandishi wetu,Arusha.

MABINGWA wa ligi kuu Tanzania bara  leo wametoka sare ya bila kufungana katika mechi ya kirafiki dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliochezwa  uwanja wa Arusha International school jijini humo.

Mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi kuu 2021/2022.

Hata hivyo mchezo wa leo ni wa kwanza  kirafiki  ikiwa ni siku nne tangu kikosi kilipowasili jijini hapo Kwa kambi ya wiki mbili.

Katika mchezo huo timu zote zilishambuliana kwa zamu na kutengeneza mashambulizi kadhaa lakini idara za ulinzi zilikuwa makini kuondoa hatari.

Pia kiungo wa klabu hiyo Bernard Morrison alionyeswa kadi nyekundu katika dakika 37 baada ya kumlipizia mchezaji wa Coastal kutokana  na kifanyiwa madhambi.

Hata hivyo benchi la ufundi chini ya kocha Didier Gomes limelidhika na viwango vya wachezaji.

Previous articleBENKI YA MWANGA HAKIKA LTD KUFANYA MKUTANO WAKE WA KWANZA WA WANAHISA SEPTEMBA18,2021
Next articleRC MAKALA AWATAKA WANANCHI WAJIEPUSHE NA MATAPELI MAGOMENI KOTA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here