Na: Stella Kessy: Dar es Salaam.
UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa umejipanga kutwaa ubingwa wa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022.
Akizungumza leo na Vyombo vya Habari, Ofisa Habari wa kikosi hicho, Masau Bwire amesema kuwa msimu huu wamefanikiwa kusajili wachezaji imara ambayo watakuwa chachu katika kuleta ushindani.
Aliongeza kuwa kikosi hicho kimesajili wachezaji 11 na kupandisha wengine watatu ambao wote ni wazawa katika nchi ya Tanzania.
“Kwa msimu huu umelenga kuchukua ubingwa na kama itashindikana basi kubaki katika nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya kimataifa.
Amesema kuwa kabla ya kuanza kwa ligi kuu msimu huu Ruvu Shooting watakuwa na usiku wa Ruvu ambao katika siku hiyo ya tarehe 25 watafanya mambo ya kijamii katika maeneo ya Kibaha na Mlandizi.
“Siku hiyo tutakuwa na wakazi wa Kibaha na Mlandizi na kushauriana nini kifanyike ili kuweza kufanikisha malengo ya timu pamoja na mbinu za kuchukua ubingwa pamoja na kufungua matawi, ” amesema
Watazindua matawi mbalimbali ambayo yapo katika mitaa mbalimbali pamoja na kuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandizi Kombaini.
Aliongeza kuwa baada ya mechi hiyo inaanza usiku wa Ruvu pamoja na kitambulisho wa wachezaji pamoja na kitambulisho wa jezi pamoja na kuwa na burudani kwa wasanii mbalimbali pamoja na bendi ya kikosi 832 bendi ambayo itatumbuiza siku hiyo.
Hata hivyo klabu hiyo imeingia udhamini na maji ya uhuru,Suma gaurd, SUMA jKt Furniture.