Home SPORTS RUVU SHOOTING YATAMBA KUBEBA KOMBE LIGI KUU MSIMU HUU

RUVU SHOOTING YATAMBA KUBEBA KOMBE LIGI KUU MSIMU HUU

Na: Stella Kessy: Dar es Salaam.

UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa umejipanga  kutwaa ubingwa wa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022.

Akizungumza leo na Vyombo vya Habari, Ofisa Habari wa kikosi hicho, Masau Bwire amesema kuwa msimu huu wamefanikiwa kusajili wachezaji imara ambayo watakuwa chachu katika kuleta ushindani.

Aliongeza kuwa kikosi hicho kimesajili wachezaji 11 na kupandisha wengine watatu ambao wote ni wazawa  katika nchi ya Tanzania.

“Kwa msimu huu umelenga kuchukua ubingwa na kama itashindikana basi  kubaki katika nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Amesema kuwa kabla ya kuanza kwa ligi kuu msimu huu Ruvu Shooting watakuwa na usiku wa Ruvu ambao katika siku hiyo ya tarehe 25 watafanya mambo ya kijamii katika maeneo ya Kibaha na Mlandizi.

“Siku hiyo tutakuwa na wakazi wa Kibaha na Mlandizi  na kushauriana  nini kifanyike ili kuweza kufanikisha malengo ya timu pamoja na mbinu za kuchukua ubingwa  pamoja na kufungua matawi, ” amesema

Watazindua matawi mbalimbali ambayo yapo katika mitaa mbalimbali pamoja na kuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Mlandizi Kombaini.

Aliongeza kuwa baada ya mechi hiyo inaanza usiku wa Ruvu pamoja na kitambulisho wa wachezaji pamoja na kitambulisho wa jezi pamoja na kuwa na burudani kwa wasanii mbalimbali pamoja na bendi ya kikosi 832 bendi ambayo itatumbuiza siku hiyo.

Hata hivyo klabu hiyo imeingia udhamini  na maji ya uhuru,Suma gaurd, SUMA jKt  Furniture.

Previous articleWAZIRI WA VIWANDA PROF. KITILA MKUMBOA ATEUA WAJUMBE SABA BODI YA NDC
Next articleSIMBA YALAMBA MKATABA MNONO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here