Na:Stella Kessy.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa ngao ya jamii utakao wakutanisha watani wa jadi klabu za Simba na Yanga utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam,
Akizungumza leo na Vyombo vya Habari msemaji wa Shirikisho la Soka la Tanzania Cliford Ndimbo,amasema viingilio vya mchezo huo ambao utaanza kutimua vumbi majira ya saa 11 kamili jioni.
Mzunguko ni 10000 ikijumlishwa viti vya blue na kijani, na Platinum hawauzi pamoja na VB 30000, VPC ,20000 na viti vya rangi ya chungwa
Aliongeza Kuwa sehemu za kuuza tiketi zitatajwa kwa pamoja na siku ya kuanza kuuza.
Huku Kwa upande wa Yanga msemaji wao Hassani Bumbuli Amesema Kuwa kikosi kimeingia kambini na kipo tayari pamoja wachezaji ambao hawakucheza katika mechi za kimataifa watacheza pamoja na waliokuwa majeruhi wapo fiti kwa ajili ya kuibuka na ushindi.
“Ninachowaomba mashabiki wajitokeze Kwa wingi katika mchezo huu wakiwa na kijiamini sababu kikosi kipo vizuri na wamejipanga vyema sababu mchezo huu Ndio kuanza kukusanya pointi za ushindi”alisema.
Kwa upande wa msemaji wa simba Ezekiel Kamwaga alisema kuwa kikosi Cha Simba kilikuwa na mapumziko ya siku mbili Baada ya kumaliza mechi dhidi ya TP Mazembe na Leo wanawasili kambini.
“Ninachoomba mashabiki wajitokeze Kwa wingi katika mchezo huo muhimu kwa Simba lengo ni kuona kikosi chao kikiwa na mwanzo mzuri dhidi ya watani wetu”alisema.