Home BUSINESS GGML YAWATAKA WADAU WA SEKTA YA MADINI KUYATUMIA MAONESHO YA MADINI KUPATA...

GGML YAWATAKA WADAU WA SEKTA YA MADINI KUYATUMIA MAONESHO YA MADINI KUPATA ELIMU

Waziri wa Madini Dotto Bitteko (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mwandamizi ushirikiano wa Taasisi za nje wa GGML Manase ndoroma (kulia) alipofika kwenye banda la Mgodi huo kujionea shughuli wanazozifanya kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayoendelea Mjini Geita. (katikati) ni Mtaalam wa Afya na Usalama wa GGML Volentine Aela.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML Richard Jordinson (katikati) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse (kushoto) pamoja na Meneja wa masuala ya kijamii Joseph Mangilima (kulia) wakati wa uzinduzi wa Ofisi za GST Mkoa wa Geita, muda mfupi kabla ya kuanza kwa ziara ya Waziri wa Madini Dotto Bitteko kutembeea mabanda ya Maonesho.

GEITA.

Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Geita Goldmining Limited (GGML) imesema kuwa ushiriki wao katika Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayoendelea kwenye uwanja wa Bombambili Mjini Geita kumeweza kuongeza tija kwa wadau wa Sekta ya madini hususani wachimbaji wadogo kwa kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Teknolojia za kisasa.

Hayo yamesemwa na Meneja Mwandamizi ushirikiano wa Taasisi za nje Manace ndoroma alipofanya mahojiano na mwandishi wa habari kuhusu ushiriki wa GGML ikiwa ni mdhanimi mkuu wa maonesho hayo kwa miaka minne mfululizo.

Ndoroma ameongeza kuwa wao kama GGML wameona maonesho hayo ni fursa ya kuendelea kutoa ujuzi wa uchimbaji wa kisasa kwa wachimbaji wadogo kuweza kunufaika ili na wao waweze kukua katika sekta hiyo.

“Haya maonesho tangu yameanza sisi tuliamini kwamba ni fursa ya kuweza  kutukutanisha na kushrikiana na wachimbaji wadogo kwa kuwapatia uzoefu, elimu na teknolojia za kisasa ili na wao waweze kukua kutoka kwenye uchimbaji mdogo na kukua ndio maana kila tukija hapa tunaleta idara zetu zote ili kuweza kutuo elimu kwa upana kulingana na vitengo mbalimbali” amesema Ndoroma.

Na kuongeza kuwa “Tunaonesha mambo ya usalama maana usalama ni tunu yetu ya kwanza sasa ili mchimbaji mdogo akue lazima achimbe kwa usalama ilimkesho pia aendelee kuwepo, tunaonesha shughuli za kiafya ili pia wajue kuwa afya ni muhimu sana kwenye masula ya uchimbaji kwahiyo vitengo vyote viko hapa tukiamini kuwa mchimbaji mdogo ana nafasi ya kukua kwa kumuangalia mchimbaji mkubwa anafanya nini” ameongeza.

Aidha ameizungumzia jamii ya wakazi wa Geita kunufaika na uwepo wa GGML ambapo amesema kuwa licha ya kodi ambayo mgodi inalipa serikalini pia kuna miradi mbalimbali ya kijamii inayotekelezwa na mgodi huo ambayo imeweza kusukuma maendeleo ya Mji huo kwa kiasi kikubwa na kuboresha maisha ya wananchi wake.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na Shule kwaajili ya kuboresha elimu za watoto wa geita, mradi mkubwa wa maji ambao umekuwa msaada mkubwa hasa kwa wakinamama wa Mji huo ambao kipindi cha nyuma wamekuwa wakisumbuka sana na suala hilo.

“Mgodi umeanzisha miradi ya kiuchumi ikiwemo ya kilimo cha kisasa cha mpunga uliopo saragurwa, na kilimo cha alizeti uliopo kasota kwa kuanzishwa kwa miradi hii ya kiuchumi itasaidia wananchi kujiongezea kipato na kuendesha maisha yao hata ikitokea siku mgodi haupo wananchi waweze kuendesha maisha yao kwa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi” amesema Ndoroma

Maonesho  hayo ya Teknolojia ya Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ni maonesho ya Nne kufanyika Mkoani Geita yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta hiyo ili kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza Teknolojia za kisasa katika sekta hiyo ikiwemo kutoa elimu kwa wadau kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ulinzi kwenye migodini.

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.TANO SEPTEMBA 22-2021
Next articleTFF YATANGAZA VIINGILIO MECHI YA SIMBA NA YANGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here