Home BUSINESS BRELA YATOA HUDUMA ZA SAJILI MAONESHO MNAZI MMOJA

BRELA YATOA HUDUMA ZA SAJILI MAONESHO MNAZI MMOJA

Msaidizi wa Usajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Athuman Makuka (kulia), akitoa elimu juu ya Usajili wa Alama ya Biashara na Huduma kwa Wadau waliotembelea banda la BRELA katika maonesho ya Wajasiliamali (Imbeju), yanayofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), inashiriki katika maonesho ya Wajasiriamali “Imbeju” na kutoa huduma za papo kwa papo za sajili mbalimbali.

Maonesho hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, yamefunguliwa rasmi leo tarehe 11 Septemba, 2023 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Katika maonesho hayo wajasiriamali wanaozalisha bidhaa mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kuonesha na kuuza bidhaa hizo huku taasisi za Serikali zikitoa huduma na elimu kwa wadau wanaotembelea maonesho hayo.
BRELA inaendelea kutoa huduma kwa wadau wanaotembelea banda hilo kwa kuwapatia elimu kuhusu huduma zinazotolewa ikiwa ni pamoja na Usajili wa Majina ya Biashara, Usajili wa Kampuni, Usajii wa Alama za Biashara na Huduma na jinsi ya kupata Leseni za Biashara kundi “A”.

Maonesho hayo yanatarajia kuhitimishwa tarehe 13 Septemba, 2023.

Previous articleNAIBU WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO KUJADILI UPATIKANAJI WA PETROL
Next articlePATA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 12 – 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here