Na Esther Mnyika Mtanzania Digital
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanganyika Flavour Limited, Alpha Nondo amesema Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika (AGRF) umewakutanisha na wadau wapya ili kubadilishana teknolojia , ujuzi na ni fursa kutangaza soko la samaki.
Akizumgumza na Mtanzania Digital Sptemba 5 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo lilipotembelea banda lililopo kwenye Ukumbi wa Mikutano Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) amesema wamefungua Kampuni hiyo mwaka 2017 ofisi inapatikana mkoani Kigoma ya kuuza samaki ndani na nje ya nchi.
Amesema lengo kubwa ni kutangaza samaki na dagaa wanaopatikana katika Ziwa Tanganyika ambao hawapatikani sehemu nyingi ili duniani itambue.
“Mkutano huu utabadilisha fikra zetu mkutano utasaidia network kila mtanzania aliyebahatika kushiriki mkutano huu atambue ni fursa ya kutangaza bidhaa na biashara yake kimataifa, “ amesema Nondo.
Amesema biashara ya samaki wanauza nchini na nchi ya Marekani wanatarajia kufungua matawi nchi nyingine na kwa mwaka huu wameingiza tani 5 za samaki nchini humo.
“Changamoto watu wa nje wanapenda samaki wa kubanikwa kutokana na changamoto hii tumebuni mashine kubwa ya kukausha samaki na dagaa kwa siku tunakausha dagaa tani kumi na samaki tani nane, ” amesema.
Aidha amesema wanashukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikiwasaidia katika mambo mbalimbali bila kikwazo chochote.