Home BUSINESS AGRF YALETA FURSA KWA WADAU SEKTA YA UVUVI NCHINI

AGRF YALETA FURSA KWA WADAU SEKTA YA UVUVI NCHINI

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanganyika Flavour Limited, Alpha Nondo amesema Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika (AGRF) umewakutanisha na wadau wapya ili kubadilishana teknolojia , ujuzi na ni fursa kutangaza soko la samaki.

Akizumgumza na Mtanzania Digital Sptemba 5 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo lilipotembelea banda lililopo kwenye Ukumbi wa Mikutano Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) amesema wamefungua Kampuni hiyo mwaka 2017 ofisi inapatikana mkoani Kigoma ya kuuza samaki ndani na nje ya nchi.

Amesema lengo kubwa ni kutangaza samaki na dagaa wanaopatikana katika Ziwa Tanganyika ambao hawapatikani sehemu nyingi ili duniani itambue.

“Mkutano huu utabadilisha fikra zetu mkutano utasaidia network kila mtanzania aliyebahatika kushiriki mkutano huu atambue ni fursa ya kutangaza bidhaa na biashara yake kimataifa, “ amesema Nondo.

Amesema biashara ya samaki wanauza nchini na nchi ya Marekani wanatarajia kufungua matawi nchi nyingine na kwa mwaka huu wameingiza tani 5 za samaki nchini humo.

“Changamoto watu wa nje wanapenda samaki wa kubanikwa kutokana na changamoto hii tumebuni mashine kubwa ya kukausha samaki na dagaa kwa siku tunakausha dagaa tani kumi na samaki tani nane, ” amesema.

Aidha amesema wanashukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikiwasaidia katika mambo mbalimbali bila kikwazo chochote.

Previous articleTANZANIA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA MAONESHO YA 68 YA VITO THAILAND
Next articleRAIS SAMIA KUZUNGUMZA NA DUNIA KUPITIA JUKWAA LA AGRF
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here