Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kuongeza muda wa udahili wa wanafunzi wanaoomba kujiunga katika masomo ya Shahada ya kwanza ya Elimu ya Juu ikiwa ni awamu ya Nne ili kutoa fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kudahiliwa katika awamu tatu zilizopita.
Akizungumza kwenye Mkutao na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa amesema kuwa hatua hiyo imefuatia baada ya kukamilika kwa udahili wa awamu tatu na kupokea maombi ya kuongeza muda wa udahili kutoka kwa Baadhi ya waombaji waliokosa udahili kutokana na sababu mbalimbali.
“Tume imepokea maombi ya kuongezea muda wa udahili kutoka kwa baadhi ya wa waombaji na Taasisi za Elimu ya Juu nchini ambazo bado zina nafasi katika baadhi ya Programu za masomo kwa mwaka 2021/2022 lengo ni kutoa fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kuomba udahili katika awamu tatu zilizopita kutokana na sababu mbali mbali kupata nafasi hiyo” Amesema Prof. Kihampa.
Aidha Tume imetoa wito kwa Taasisi za Elimu ya Juu nchini zilizoidhinishwa kudahili kwa mwaka huuwa masomo wa 2021/2022 kutangaza programu zile zenye nafasi tu ili wa waombaji waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wakituma maombi na kuepuka usumbufu kwa wao mbaji kuomba programu ambazo hazina nafasi.
“Kama tume pia tunasisitiza vyuo vyote kuzingatia idadi ya wanafunzi iliyoidhinishwa katika programu husika na kwa waombaji wote wanakumbushwa masuala yote yanayohusiana na udahili ama kujithibitisha yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo na siyo TCU,” amesema Profesa Kihampa
Amewakumbusha waombaji wote kuwa masuala ya yanayohusiana na udahiliama kuthibitisha yawasilishwe moja kwa moja katika vyuo husika na si TCU.