Home SPORTS STARS YAREJEA DAR KIBABE

STARS YAREJEA DAR KIBABE

Mwandishi wetu.

TIMU ya taifa ya Tanzania,  Taifa Stars imewasili leo ikitokea nchini Benin ambapo ilikuwa na mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

kikosi hicho cha Stars jana  ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0  dhidi ya Benin na kukusanya pointi tatu muhimu.

Ushindi huo ambao stars wamepata imewaweka katika nafasi nzuri  katika michuano hiyo ya kuwania kufuzu kombe la dunia.
Hata hivyo kikosi hicho ambacho kilipoteza nyumbani kwa kichapo cha  bao 1-0  mchezo uliochezwa katika  Uwanja wa Mkapa.

Simon Msuva ambaye alipachika bao la ushindi dakika ya 6 na kuifanya Stars kuwa namba moja katika kundi J ikiwa na pointi 7 sawa na Benin iliyonafasi ya pili.

Msuva ambaye alikuwa na furaha kubwa sawa na wachezaji wengine amesema kuwa ushindi ni zawadi kwa Watanzania.

“Ushindi ambao tumeupata ni zawadi kwa Watanzania kwa kuwa tunapambana kwa ajili ya nchi hivyo ni zawadi kwao nasi tumetimiza majukumu yetu,”

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!