Mtendaji Mkuu Wakala wa Chakula Tanzania (NFRA) CPA. Milton Lupa akijadiliana jambo na Afisa Uhusiano NFRA Bi. Angela Shangali katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya kuhusu ununuaji wa nafaka mwaka huu wa fedha 2023/2024.
Bw. Simon Bikaru Afisa Masoko (NFRA) akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea katika banda la hilo kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya JohnMwakangale jijini Mbeya.
Picha mbalimbali zikionesha watumishi wa Wakala wa Chakula Tanzania (NFRA) wakitoa elimu kwa wananchi mbalimbali waliotembelea katika banda hilo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Na: Mwandishi wetu, MBEYA
Wakala wa chakula nchini NFRA wametoa wasiwasi wananchi kuhusu Hali ya chakula na kusema kuwa chakula kipo Cha kutosha.
Akizungumza kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Mtendaji Mkuu wa NFRA Bw. Milton Lupa amesema Tanzania inachakula cha kutosha kutumika ndani ya nchi na kuuza nje huku ikiendelea na ununuzi wa chakula kingine.
Amesema uwepo wao kwenye maonyesho hayo pamoja na kuonyesha shughuli zao lakini pia kuwaonyesha wakulima vigezo vinavyotumika katika ununuzi wa mazao katika masoko ya ndani na nje.
“Nafaka tunazozinunua sisi ni Mahindi,Mpunga na Mtama na vigezo tunavyovitumia ndio hivyo vinavyotumika kimataifa hivyo tunawakaribisha Wakulima kuja kutembelea kwenye Banda letu ili wajifunze vigezo wakipeleka mazoa yao nje wasirudishiwe”amesema Lupa.
Akitaja vigezo hivyo amesema kigezo kikubwa kinachoangaliwa ni ukaukaji wa nafaka kwa asilimia 13.5 hivyo kama mahindi hayajakauka Kwa kiwango hicho ukiyahifadhi yanaharibika.
Amesema kigezo kingine ni maozeo ambapo NFRA wanaruhusu mwisho Asilimia 2 Kwani yakiwa zàidi ya hapo yatakataliwa.
“Ameongeza kuwa kigezo kingine ni harufu ambapo ukienda kupima ya yakitoa harufu yatakakataliwa.
“Biashara ya nafaka ndio imekua biashara kubwa Duniani hivyo wananchi lazima wafuate vigezo vya chakula ambacho ni Bora na ndio maana tupo hapa Kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi,”ameongeza Lupa