Home BUSINESS CPA. MILTON LUPA: TUNA CHAKULA CHA KUTOSHA NCHINI

CPA. MILTON LUPA: TUNA CHAKULA CHA KUTOSHA NCHINI

Mtendaji Mkuu Wakala wa Chakula Tanzania (NFRA)  CPA. Milton Lupa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya kuhusu ununuaji wa nafaka  mwaka huu wa fedha 2023/2024.

Mtendaji Mkuu Wakala wa Chakula Tanzania (NFRA)  CPA. Milton Lupa akijadiliana jambo na Afisa Uhusiano NFRA Bi. Angela Shangali katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya kuhusu ununuaji wa nafaka  mwaka huu wa fedha 2023/2024.

Bw. Simon Bikaru Afisa Masoko (NFRA) akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea katika banda la  hilo kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo  Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya JohnMwakangale jijini Mbeya.

Picha mbalimbali zikionesha watumishi wa Wakala wa Chakula Tanzania (NFRA) wakitoa elimu kwa wananchi mbalimbali waliotembelea katika banda hilo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Na: Mwandishi wetu, MBEYA

Wakala wa chakula nchini NFRA wametoa wasiwasi wananchi kuhusu Hali ya chakula na kusema kuwa chakula kipo Cha kutosha.

Akizungumza kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo  Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Mtendaji Mkuu wa NFRA Bw. Milton Lupa amesema Tanzania inachakula cha kutosha kutumika ndani ya nchi na kuuza nje huku ikiendelea na ununuzi wa chakula kingine.

Amesema uwepo wao kwenye maonyesho hayo pamoja na kuonyesha shughuli zao lakini pia kuwaonyesha wakulima vigezo vinavyotumika katika ununuzi wa mazao katika masoko ya ndani na nje.

“Nafaka  tunazozinunua sisi ni Mahindi,Mpunga na Mtama na vigezo tunavyovitumia ndio hivyo vinavyotumika kimataifa hivyo tunawakaribisha Wakulima kuja kutembelea kwenye Banda letu ili wajifunze vigezo wakipeleka mazoa yao nje wasirudishiwe”amesema Lupa.

Akitaja vigezo hivyo amesema kigezo kikubwa kinachoangaliwa ni ukaukaji wa nafaka kwa asilimia 13.5 hivyo kama mahindi hayajakauka Kwa kiwango hicho ukiyahifadhi yanaharibika.

Amesema kigezo kingine ni maozeo ambapo NFRA wanaruhusu mwisho Asilimia 2 Kwani yakiwa zàidi ya hapo yatakataliwa.

“Ameongeza kuwa kigezo kingine ni harufu ambapo ukienda kupima ya yakitoa harufu yatakakataliwa.

“Biashara ya nafaka ndio imekua biashara kubwa Duniani hivyo wananchi lazima wafuate vigezo vya chakula ambacho ni Bora na ndio maana tupo hapa Kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi,”ameongeza Lupa

Previous articleNSSF YASHIRIKI NANENANE KITAIFA NA KIMKOA -YAHIMIZA WANANCHI KUJIUNGA NA KUCHANGIA NSSF
Next articleMKURUGENZI MKUU VETA: UJUZI WANAOUPATA WANAFUNZI WETU NI WA KIPEKEE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here