MCHEZO kati ya DTB na Ndanda umesogezwa mbele ili kupisha mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati y Simba na Red Arrow zitakazochezwa Novemba 29 katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo wa DTB utachezwa Novemba 29 katika dimba la uhuru jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DTB, Juma Ayo amesema kuwa mchezo huo umepelekwa mbele kupisha mchezo wa kimataifa kati ya Simba dhidi ya Red Arrows utakaochezwa Uwanja wa Mkapa ambao ni wa Kombe la Shirikisho.
“Mchezo wetu dhidi ya Ndanda FC uliopangwa kuchezwa Novemba 28 umepelekwa mbele mpaka Novemba 29 Uwanja wa Uhuru,pia.
Sababu za kusogezwa mbele ni kupisha mchezo wa kimataifa kati ya Simba na Red Arrows utakaochezwa Novemba 28,Uwanja wa Mkapa.
”Mashabiki wa DTB tunaomba radhi kwa mabadiliko haya,tujitokeze kwa wingi siku husika kwa ajili ya kuishangilia timu yetu,” amesema.
DTB ni namba moja kwenye ligi wakiwa na jumla ya pointi 18 baada ya kucheza mechi 8 msimu huu wa 2021/22