Home SPORTS DTB Vs NDANDA KUCHUANA NOVEMBA 29

DTB Vs NDANDA KUCHUANA NOVEMBA 29


Na: Stella kessy 

MCHEZO  kati  ya DTB na Ndanda umesogezwa mbele ili kupisha mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati y Simba na Red Arrow zitakazochezwa Novemba  29 katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa  DTB utachezwa  Novemba 29  katika dimba la uhuru jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DTB, Juma Ayo amesema kuwa mchezo huo umepelekwa mbele kupisha mchezo wa kimataifa kati ya Simba dhidi ya Red Arrows utakaochezwa Uwanja wa Mkapa ambao ni wa Kombe la Shirikisho.

“Mchezo wetu dhidi ya Ndanda FC uliopangwa kuchezwa Novemba 28 umepelekwa mbele mpaka Novemba 29 Uwanja wa Uhuru,pia.

Sababu za kusogezwa mbele ni kupisha mchezo wa kimataifa kati ya Simba na Red Arrows utakaochezwa Novemba 28,Uwanja wa Mkapa.

”Mashabiki wa DTB tunaomba radhi kwa mabadiliko haya,tujitokeze kwa wingi siku husika kwa ajili ya kuishangilia timu yetu,” amesema.

DTB ni namba moja kwenye ligi wakiwa na jumla ya pointi 18 baada ya kucheza mechi 8 msimu huu wa 2021/22

Previous articleSIMBA YAZIDI KUJINOA DHIDI YA RED ARROWS
Next articleWARATIBU WA MIKOA WA TIBA ASILI/MBADALA WAJENGEWA UWEZO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here