Home SPORTS SIMBA YAZIDI KUJINOA DHIDI YA RED ARROWS

SIMBA YAZIDI KUJINOA DHIDI YA RED ARROWS

Na Stella Kessy, Mwandishi wetu

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya kuivutia kasi Red Arrows katika mchezo wao wa kimataifa.

Mtanange huo utachezwa Novemba 29 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kusaka ushindi ndani ya dakika 90.

Hata hivyo Simba imeangukia hatua ya Kombe la Shirikisho baada ya kuangukia pua katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwa ilinyooshwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa na kuondolewa mazima.

Licha ya kwamba mchezo wa kwanza ugenini ilishinda mabao 2-0 imeondolewa kwa idadi ya kufungwa mabao mengi nyumbani.

Akizungumza kocha mkuu wa timu ya Simba Pablo Franco amesema kuwa mchezo dhidi ya Red Arrows utakuwa mgumu na wachezaji wanapaswa kujitoa asilimiab100 katika muda wote wa dakika 90 za machezo.

“Kwakweli Mechi itakuwa ngumu , tupo nyumbani inatupasa kujituma kwa asilimia 100 muda wote wa mchezo ili tupate ushindi, maandalizi yanaendelea vizuri na matarajio yetu ni kupata ushindi “amesema

Previous articleUIMARISHAJI SEKTA YA AFYA WATAWALA MKUTANO WA 22 WA MAPITIO YA PAMOJA YA SERA YA MWAKA
Next articleDTB Vs NDANDA KUCHUANA NOVEMBA 29
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here