Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji Saini Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika kipande cha tatu cha mradi huo (Lot III). Wa kwanza (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli nchini (TRC) Bw. Masanja Kadogosa akiweka saini moja ya Kitabu cha Mkataba huo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkez ya Uturuki Bw. Erdem Arioglu katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Desemba 2021.
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli nchini Bw. Masanja Kadogosa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkez ya Uturuki Bw. Erdem Arioglu wakibadilishana Vitabu vya Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika awamu ya tatu ya mradi huo (Lot III).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika kipande cha tatu cha mradi huo (Lot III). wa kwanza, hafla hiyo imefanyika leo tarehe 28 Desemba 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.