Home LOCAL MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI WA...

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR) KUTOKA MAKUTUPORA (SINGIDA) HADI TABORA KM 368

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji Saini Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika kipande cha tatu cha mradi huo (Lot III). Wa kwanza (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli nchini (TRC) Bw. Masanja Kadogosa akiweka saini moja ya Kitabu cha Mkataba huo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkez ya Uturuki Bw. Erdem Arioglu katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Desemba 2021.
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli nchini Bw. Masanja Kadogosa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkez ya Uturuki Bw. Erdem Arioglu wakibadilishana Vitabu vya Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika awamu ya tatu ya mradi huo (Lot III).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika kipande cha tatu cha mradi huo (Lot III). wa kwanza, hafla hiyo imefanyika leo tarehe 28 Desemba 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.


Previous articleSIMBA YAPANGWA KUNDI MOJA NA TIMU YA CHAMA, TUISILA SHIRIKISHO
Next articleTAKRIBANI WAFANYABIASHARA 350 KUTOKA NCHI MBALIMBALI WANATARAJIWA KUSHIRIKI TAMASHA LA BIASHARA LA ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here