Home BUSINESS TAKRIBANI WAFANYABIASHARA 350 KUTOKA NCHI MBALIMBALI WANATARAJIWA KUSHIRIKI TAMASHA LA BIASHARA LA...

TAKRIBANI WAFANYABIASHARA 350 KUTOKA NCHI MBALIMBALI WANATARAJIWA KUSHIRIKI TAMASHA LA BIASHARA LA ZANZIBAR

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaabani akizungumza na waandishi wa habari Kuhusu tamasha la nane la Biashara ambalo litaanza Januari 2 Hadi Januari 15 katika Viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini , ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za kusherehekea miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,hafla hiyo ilifanyika Ofisi za Wizara ya Biashara Malindi.

Na: Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar . 28/12/2021.

Kiasi ya Wafanyabiashara 350  kutoka nchi mbali mbali wanatarajiwa kushiriki Tamasha la biashara la Zanzibar  linalotarajiwa kuanza Januari 02 hadi Januar 15 mwaka 2O22 katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini . .

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban ameyasema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Malindi .

Amesema tamasha hilo litatoa fursa za kibiashara, kuongeza ujuzi na wigo kwa wajasiriamali wadogo wadogo wenye viwanda pamoja na Taasisi za Serikali zinazotoa huduma mbali mbali kwa jamii.

Alisema ni miaka minane  tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo, kupitia Wizara ya Biashara ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra ya maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar .

Nchi zinazotarajiwa kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Uganda,Kenya, Misri, Burundi , Tanzania bara na wenyeji Zanzibar ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Teknolojia na Ubunifu katika ukuaji wa Biashara .

lengo ni kukuza biashara kwa kutumia teknolojia ya kuuza na kununua bidhaa kwa njia ya mtandao na wajasiriamali wachanga kutumika na kuengezeka thamani .

Hata hivyo aliwataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la nane la biashara la Zanzibar kwa  kununua bidhaa zenye ubora za ndani na nje ya nchi .

Previous articleMHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR) KUTOKA MAKUTUPORA (SINGIDA) HADI TABORA KM 368
Next articleTAMCU LTD YASAMBAZA VIFAA KWA KUPIMIA UNYEVU WA KOROSHO KWA VYAMA VYA MSINGI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here