Mtendaji mkuu wa mawsiliani kwa wote mwanasheria Justina Mashimba Akizungumza na wananchi waliohuduria uzinduzi huo.
Mbunge wa jimbo la Igalula, Venant Daudi akizungumza mbele ya Naibu waziri wa habari ,mwasiliano na teknolojia ya habari Mhandisi Kundo Mathew
Na Lucas Raphael,Tabora.
Naibu waziri wa habari ,mwasiliano na teknolojia ya habari Mhandisi Kundo Mathew ameyataka Makampuni ya simu nchini kuendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha maeneo yenye changamoto za mawasiliano yanafikia wananchi walio wengi ambapo uligharimu kiasi cha shilingi Milioni 300 .
Akizungumza katika hotuba yake kwenye uzinduzi wa mnara wa Mawasiliano ya simu ya kampuni ya airtel katika kijiji cha Magulyati kata ya loya wilaya ya Uyuni Mkoani Tabora
Alisema kwamba huduma za mwasiliano za simu ,ujenzi wa minara uende sambamba na matumizi ya kisasa na teknolojia ya kisasa yenye uwezo wa kutoa huduma ya internet.
Naibu waziri huyo alisema kampuni hiyo ihakikishe inasimamia mnara huo na kutoa huduma kwa wakati wote ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za mawasiliano ya simu muda wote.
Aidha Mhandisi Kundo alisema kwamba Serikali ya awamu ya sita inatambua umuhimu wa kupeleka huduma za mawasiliano sehemu zenye mawasiliano hafifu na upelekaji huo wa huduma uendelee kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yanayofikiwa na huduma .
Hata hivyo aliwahakikishia kuwa serikali inathamini mchango wa makampuni ya simu kwa kuyafikia maeneo yenye changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa miundombinu wezeshi kama umeme na barabara.
“Watoa huduma ni muhimu sana katika kutoa huduma bora na ni wazi kuwepo kwa miundombinu hivyo ingepunguza gharama za uendeshaji wa miundombinu yenu ya mawasiliano “alisema Naibu Waziri.
Alisema kwamba serikali inatambua kuwa mfuko wa maasiliano kwa wote (UCSAF) unatoa ruzuku ambavyo ni sehemu ya gharama nzima ya miundombinu ya mawasiliano wakati ambapo hali halisi ni kubwa zaidi.
Kwa upande Mtendaji mkuu wa mawsiliani kwa wote mwanasheria Justina Mashimba alisema kwamba , Serikali ilianzisha mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ,lengo ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma za mawasilano ya simu ,Televisheni na radio katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mjini yenye huduma hafifu za mawasiliano.
Alisema Serikali kupitia mfuko wa mawasiliano ,imejenga mnara wa simu kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel katika kijiji hicho kata ya Loya na Migowa ili kuhakikisha wananchi wa vijiji hivyo wanapata huduma ya mawasiliano ya simu.
Alisema kwamba mfuko huo unaendelea na miradi 19 kwenye maeneo ya mkoa wa Tabora ikiwemo wilaya ya Uyui ambayo itaanza kutekelezwa hivi karibuni.
Mbunge wa jimbo la Igalula, Venant Daud alimtaka Naibu waziri wa habari na mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote kuyapatia maeneo mengine ya wilaya humo Mawasiliano ya simu ili kuwezesha kujiinua kiuchumi.
Alisema kwamba huduma ya mawasiliano ya simu ni muhimu katika kuwezesha wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii .
Alisema kwamba mawalisiliano ya simu ni nyenzo muhimu katika kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za maendeleo kwani huwezesha mtiririko na kubadilishana habari kwa haraka .
Mwisho.