Home LOCAL NAPE AWATAKA WANAHABARI KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO 

NAPE AWATAKA WANAHABARI KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO 

Waziri wa habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amewataka Wanahabari nchini kutumia vema kalamu zao kwa kuandika habari zinachochea ukuaji wa maendeleo katika Sekta mbalimbali hapa nchini.

Waziri Nape amesema hayo wakati akifungua kongamano la maendeleo ya Sekta ya habari  mwaka  2022 lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JKNCC Disemba 17 Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa wanahabari wananafasi kubwa katika kuchochea maendeleo ya ukuaji wa Sekta mbalimbali nchini.

Amewataka wanahabari kuandika makala zitakazochochea maendeleo ya kisekta ikiwemo uvuvi, kilimo na ufugaji endelevu kwa lengo la kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi.

“Maendeleo yoyote katika nchi yanachagizwa na Sekta ya habari kwa kuandika habari zinazogusa sekta mbalimbali kwa lengo la kuchochea na kukuza uchumi wa Taifa”

“Hivyo Wana habari ni vema kujielekeza kuandika habari hzo. Kwa kufanya hivyo mtakuwa mmefanya kazi nzuri ya kuuhabarisha umma wa watanzania  pamoja na kulinda taifa  kwa ujumla” amesema Waziri Nape.

Aidha Waziri huyo ametumia Kongamano hilo kuwahakikishia waandishi na wadau wote wa habari nchini kuwa Serikali itahakikisha kuanzia mwaka ujao 2023 haki na stahiki za wanahabari zinaboreshwa ikiwemo Masuala ya mikataba, sambamba na kuimarisha uchumi wa vyombo vya habari kwa kuhakikisha madeni yao yanalipwa.

Kongamano hilo la siku moja liliwakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya habari Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na mashirika  ya umoja wa Mataifa likiwa limebebwa na kaulimbiu ya ‘Habari kwa Maendeleo endelevu’

Previous articleSHERIA YA HABARI IKIREKEBISHWA UHURU WA HABARI UTAPATIKANA – BALILE
Next articleRAIS SAMIA KUZINDUA ZOEZI LA UJAZAJI MAJI BWAWA LA KUFUA UMEME LA JULIUS NYERERE 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here