Home LOCAL SHERIA YA HABARI IKIREKEBISHWA UHURU WA HABARI UTAPATIKANA – BALILE

SHERIA YA HABARI IKIREKEBISHWA UHURU WA HABARI UTAPATIKANA – BALILE

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amesema marekebisho ya sheria ya huduma za habari yatasaidia kwa kiasi kikubwa kulindwa kwa uhuru wa habari hapa nchini.

Balile amebainisha hayo alipokuwa akizungumza katika kongamano la maendeleo ya Sekta ya habari  mwaka 2022 lililofanyika Disemba 17 mwaka huu Katika ukumbi wa JKNCC Jijini Dar es Salaam ambapo amesema vyombo vya habari vilikuwa kwenye kitanzi lakini kwa sasa kuna uhuru ambao unapaswa kulindwa kisheria kwa kufanyika marekebisho katika sheria zilizopo.

Amesema Serikali ya awamu ya sita imesadia kulegeza ugumu uliokuwa unaikabili sekta hiyo na kuvifanya vyombo vya habari kutokuwa huru katika utendaji kazi wake.

“Kuna wakati sheria kwenye sekta ya habari zilikuwa kitanzi magazeti yalifungiwa na uhuru ukapotea kabisa ilivyokuja Serikali ya awamu ya sita, yamefanyika maboresho makubwa Rais aliondoa mtanziko uliokuwepo, sasa hivi tuna raha kwa kweli” .

Ameongeza kwa  kusema wadau wa sekta ya habari hivi sasa wanafurahia kiwango cha uhuru wa habari kilichopo hapa nchini lakini uhuru huo utalindwa kisheria pale mabadiliko hayo yatakapofanyika.

Aidha Bale amemuomba Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kutia nguvu kwenye madeni ya vyombo vya habari kwa Serikali ambapo hadi kufikia mwaka jana jumla ya Sh18 bilioni zilikuwa zinadaiwa.

Amesema licha ya halmashauri ya katibu mkuu wa TAMISEMI kuziandikia barua Halmashauri zinazodaiwa nya vyombo vya habari mbalimbali lakini zimeshindwa kulipa madeni hayo licha kuelekezwa kulipa.

Previous articleFAMILY DAY YA MGODI WA NORTH MARA YAKUTANISHA FAMILIA ZA WAFANYAKAZI NA JAMII INAYOISHI NA MGODI KUFURAHI PAMOJA
Next articleNAPE AWATAKA WANAHABARI KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here