Home LOCAL RAIS SAMIA KUZINDUA ZOEZI LA UJAZAJI MAJI BWAWA LA KUFUA UMEME LA...

RAIS SAMIA KUZINDUA ZOEZI LA UJAZAJI MAJI BWAWA LA KUFUA UMEME LA JULIUS NYERERE 

Na: Beatrice Sanga-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio la kushuhudia ufungaji wa lango la handaki mchepuko (diversion tunnel) ili kuruhusu maji kuanza kujaa katika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere litakalofanyika siku ya Alhamis, Tarehe 22 Disemba 2022

Akizungumza na waandishi wa Habari katika eneo la mradi wa umeme wa Mto Rufiji Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amesema mradi huo unahatua kubwa mbili ambazo Zina hadhi ya kushuhudiwa na kusherehekewa ambapo hatua ya kwanza ni kufunga lango la njia ya mchepusho wa maji na ya pili ni kuwasha mitambo ya kufua umeme

“Kwa ujumla hadi Leo mradi huu umefikia hatua ya asilimia 78, ni hatua kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na katika hatua za mradi, mradi huu unaa maisha na Kuna Alama ambazo tunafikia siku zote na hatua zote ni muhimu”

“Tumemaliza kujenga tuta, barabara, tumemaliza kujenga nyumba za wafanyakazi kwahiyo Kuna mafanikio katika kipindi chote, sasa tumefikia kwenye mafanikio makubwa tangu tuanze ujenzi wa mradi huu na yenyewe ni kujaza maji kwenye bwawa , kazi ya kujenga handaki la kuchepusha maji ilifanyika miaka mitatu iliyopita na handaki Hilo Lina urefu wa mita 700 na ujenzi uligharimu sh bil 235” amesema Mhe. Makamba

Mhe. Makamba amesema kuwa kutokana na umuhimu wa hatua hiyo ya mradi ulipofikia hatua hii ya kuanza kujaza maji kwenye bwawa itazinduliwa na na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Tar 22 Disemba 2022 siku ya Alhamisi ambapo Mheshimiwa Rais atabonyeza kitufe ambacho kitashusha geti la kuziba handaki lilikuwa linachepusha maji na rasmi maji yataanza kujaa kwenye bwawa

Ameongeza kuwa Shughuli hiyo itauzuliwa na watu takribani 2000 wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na viongozi wengine kama spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mawaziri, Makatibu Wakuu, wakuu wa Mikoa na Wilaya zinazozunguka Bonde la mto Rufiji, viongozi wa Dini, Viongozi wa Chama na wananchi, lakini pia serikali ya Misri ambapo ndipo wanatoka wakandarasi wanaojenga mradi huo, mawaziri, viongozi we serikali pamoja na vyombo vya Habari vya nchi hiyo watahudhuria wakiongozwa na waziri wa mambo ya nje nchini Misri.

Akizungumzia faida za mradi huo Mh. Makamba amesema ndani ya Serikali mradi huu ni mpana zaidi na utasaidia pia katika masuala ya Kilimo chini ya mto Rufiji, Uvuvi, Kuondoa mafuriko, Upatikanaji wa huduma za maji wa uhakika kwa Jiji la Dar es Salaam, Utalii, miundombinu na usafirishaji pamoja na kupata umeme wa uhakika.

Naye Mkurugenzi wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Maharage Chande ameeleza kuwa inakadiriwa kwamba misimu miwili ya mvua itaweza kufanya bwawa Hilo la Julius Nyerere kujaa maji hivyo zinatazamiwa mvua za masika Machi 2023 na 2024 kuweza kujaza Bwawa hilo.

Mradi wa kufua umeme kwa njia ya maji wa Julias Nyerere amamba unakadiriwa kuzalisha megawati 2115, ulianza kujengwa mwaka 2019 na unatarajiwa kukamilika June 2024 na umegharimu kiasi cha Shilingi Trilion 6.5 ukiwa umebakisha asilimia 22 mpaka kukamilika

MWISHO

Previous articleNAPE AWATAKA WANAHABARI KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO 
Next articleSIMBA SC YAICHAKAZA GEITA GOLD 5-0 KILUMBA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here