Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita kamishina msaidizi Henry Mwaibambe amewataka waendesha Bajaji pamoja na pikiki maarufu kama Bodaboda kuachana na ukatili wa kijinsia kwa watoto pindi wanapofanya shughuli zao za usafirishaji.
Ametoa rai hiyo wakati akihitimisha mafunzo juu ya ukatili wa wakijinsia kwa watoto yaliyotolewa na shirika la Plan international kwa mwendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda 200 kwa mda wa siku tatu mkoani Geita.
Kamanda Mwaibambe amesema kuna kesi kazaa katika jesho la polisi za ukatilii wa kijinsia kwa watoto ambapo amesema watuhumiwa ni madereva bajaji pamoja na Bodaboda, amewataka kuacha mara moja kufanya hivyo kwani nikinyume na sheria za nchi.
Amesema wale wote wanaobainika kufanya ukatili wa kijinsia kwa watoto, wao kama jeshi la polisi wanawachukulia hatua haraka iwezekanavyo kwa mjibu wa sheria ili kukomesha ukati wa kijinsia kwa watoto.
Mwaibambe amelipongeza shirika la Plan international kwa kutoa elimu hiyo kwa waendesha piki piki maarufu kama boda boda huku akiwataka pia wasiishie hapo watoe pia elimu hiyo kwa waendesha bajaji kwani ni kundi jipya ambalo limeibuka kwa kasi katika kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto.
“Semina hii ya watu wa plam tuwashukuru kwa semina ya hawa bodaboda tusibeze kwa bodaboda peke yao tubeze hata hawa bajaji, bajaji sasa ndo inaonekana ni shida tumegundua bajaji sasa ni eneo hatalishi kwa mambo ya ukatili wa kijinsia watoto wengi wanafanyiwa ukatili kwenye bajaji au bajaji inatumika kubeba” Amesema Mwaibambe.
Kwa upande wake Mratibu miradi shirika la plan International mkoa wa Geita Zamda Magowa amesema elimu walioitoa kwa wendesha pikipiki imekuwa na tija kubwa katika mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watoto ndani ya mkoa wa Geita kwani wamewapa elimu ya kutosha juu ya athali za ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Zamda amemuhakikishi kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita kamishina msaidizi Henry Mwaibambe kutoa elimu hiyo kwa kundi la waendesha bajaji ambalo kwa sasa linaonekana kuwa changamoto kubwa katika kuwafanyaia ukatili wa kijinsia watoto.
Aidha Zamda ameitaka jamii kuungana kwa pamoja kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watoto kwani ukatili wa kijinsia una athali kubwa kwa watoto ikiwemo kusababisha kifo,ulemavu, pamoja na watoto kujitenga katika jamii.
“Ukatili una athali kubwa kwa watoto wetu unaleta athali za vifo, unaacha ulemavu watoto wanakuwa wanyonge watoto wanajitenga kwahiyo sasa ni wakati tuungane kwa pamoja wote dhidi ya vita hivi vya ukatili wa kijinsia na ukatili kwa watoto” Amesema Zamda Magowa.
Renatus Gilbelt ambaye ni mwendesha Bodaboda ni miongoni wa madereva 200 waliopata elimu juu ya ukatili wa kijinsia amesema elimu waliyoita imewafungua juu ya athali za ukatili wa kijinsia na kuahidi kuwa msitari wa mbele katika mapambano ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Renatus amesema kutokana na elimu waliyopewa na shirika la Plan international juu ya ukatili wa kijinsia kwa watoto, wataitumia elimu hiyo kuwaelimisha madereva ambao hawakuweza kupata nafasi ya kuhudhulia mafunzo hayo hivyo wao kama bodaboda watakuwa mabalozi wazuri katika kutoa elimu pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto ndani ya mkoa wa Geita.