Justine Katiti Afisa wa Huduma kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Geita
Na. Costantine James, Geita.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita Imewataka wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara zao pamoja na kutoa risiti kwa kutumia EFD mashine kwa kila mauzo wanayoyafanya ili kujua mwenendo wa biashara zao kwa lengo la kulipa kodi stahiki.
Hayo yamebainishwa na Afisa wa Huduma kwa Mlipakodi kutoka TRA Mkoa wa Geita Bw. Justine Katiti wakati wa semina na Wafanyabiashara wa Muganza,Wilaya Ya Chato Mkoani Geita.
Bw.Katiti amewataka wafanyabiashara hao ambao bado hawajajisajili biashara zao wafike TRA Mkoa wa Geita ili waweze kusajili biashara zao kwa lengo la kutekeleza matakwa ya kisheria ili kuepuka adhabu.